Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

M-Pesa

M-pesa ni huduma ya Safaricom. Huduma hii inakuruhusu kuweka pesa katika akaunti maalum, kutuma na kupokea pesa, kulipia bili na pia kununua pesa za mawasiliano kwa kutumia simu yako.

Nitapataje akaunti ya Mpesa?
Kadi zote za simu za safaricom zina sehemu ya Mpesa. Yawezekana usiwe na sehemu ya Mpesa iwapo kadi yako ni mzee. Ndipo ujiandikishe, nenda kwa ejenti yeyote wa Mpesa na simu yako na kitambulisho chako.
 
Kuweka na kutuma pesa
Waweza kutuma pesa hadi kwa simu nyingine yoyote nchini Kenya. Ili ufanye hivyo ni sharti kwanza uweke pesa katika akaunti yako ya Mpesa. Unafanya hivyo kwa kuenda kwa ajenti wa Mpesa ambaye atakuwekea pesa hizo kwa simu yako.
Ni nini unachohitaji ili uweke fedha katika akaunti yako ya Mpesa?
 • Nenda kwa ejenti wa Mpesa aliyesajiliwa na simu yako na kitambulisho chako.
 • Mweleze ejenti huyo ni pesa ngapi ungependa kuweka; halafu umpatie. 
 • Watatumia simu yao ya maajenti kukutumia fedha
 • Wewe na ejenti wa Mpesa mtapokea ujumbe wa kuhakikisha kuwa pesa zimewekwa.
Kutuma pesa nenda kwa sehemu ya ‘safaricom’ kisha uchague M-PESA.
 • Chagua ‘Tuma Pesa’
 • Ingiza nambari ya mpokezi wa hizo pesa, kiwango cha pesa na nambari yako ya siri.
 • Utaonyeshwa ujumbe wako jinsi ulivyouandika, hakikisha uko sawa kasha ubonyeze ‘OK’
Nitafanyaje iwapo nitazituma pesa kwa nambari isiyofaa? 
 • Piga nambari 234 mara moja kasha upeane nambari ambayo imepokea pesa hizo kwa bahati mbaya.
 • Pesa zilizotumwa kwa nambari isiyofaa zitarudishwa tu kama bado ziko katika akaunti ya aliyezipokea.
 • Ukifaulu utapokea ujumbe kukuarifu kuwa pesa zimerejeshwa.
Kutoa pesa
Waweza kutoa pesa kutoka kwa ajenti yeyote wa Mpesa au kutoka kwa ATM ya Pesapoint. Iwapo umesajiliwa na Mpesa nenda kwa ejenti wa Mpesa kisha:
 • Muulize ejenti kama ana fedha za kutosha zile unazotaka kutoa.
 • Peana nambari yako ya simu na uonyeshe kitambulisho chako cha kitaifa.
 • Nenda katika orodha yako ya Mpesa na uchague ‘Toa Pesa’
 • Ingiza nambari ya ejenti, kiasi cha pesa unachotaka kutoa na nambari yako ya siri.
 • Dhibitisha kuwa uliyoyaandika ni sawa kasha bonyeza OK
 • Wewe na ejenti mtapataujumbe wa kuonyesha kuwa mkataba wa pesa umetekelezwa.
 • Ejenti baadaye atakupa fedha na kukuhimiza uweke sahihi katika kitabu ambacho hutumika kuweka rekodi za pesa za ejenti huyo.
Iwapo hujasajiliwa, nenda kwa ejenti wa Mpesa kisha:
 • Uliza iwapo kuna fedha za kutosha
 • Onyesha SMS iliyo na nambari ya Mpesa( inayoonyesha kuwa umepokea fedha)
 • Peana nambari yako ya simu na uonyeshe kitambulisho cha kitaifa.
 • Ejenti atainakili nambari iliyoko kwa ujumbe mfupi wa mteja.
 • Ejenti na mteja wote watapokea ujumbe mfupi kudhibitisha
 • Ejenti atakupa pesa zako kasha utaweka sahihi katika kitabu chake anachowekea rekodi za biashara.
Pia waweza ukatoa pesa kutoka kwa mtambo wa PesaPoint ATM. Wateja walioandikishwa tu ndio wanaoweza kutumia mpangilio huu. Kutoa pesa ni sharti ufuate masharti kwa simu yako na kwa mtambo wa PesaPoint.
Mwanzo kwenye simu yako:
 • Chagua ATM withdrawal kutoka kwa orodha ya Mpesa
 • Ingiza nambari ya Pesapoint (555 555)
 • Ingiza nambari yako ya siri ya Mpesa
 • Utapokea ujumbe mfupi kutoka kwa Mpesa ulio na nambari 6. Ujumbe huu hauna maana baada ya masaa mawili hivyo basi utalazimika kuanza tena iwapo unataka kuzitoa pesa.
Kwenye ATM
 • Chagua kipengele cha M-PESA kwenye mtambo wa PesaPoint
 • Chagua lugha uitakayo
 • Finya nambari 6 za kukuruhusu kutumia mtambo wa Pesapoint.
 • Weka nambari yako ya simu ya Safaricom.  
 • Weka kiasi cha pesa ungetaka kutoa halafu bonyeza ENDELEA
 • Mtambo wa ATM utakutolea pesa zako na risiti ya utaratibu. Utapata ujumbe mfupi – SMS kudhibitisha utaratibu.
Kutoa pesa za kupiga simu
Iwapo wewe ni mteja wa M-PESA uliyesajiliwa waweza kununua muda wa maongezi kutoka Ksh.20 hadi Ksh 10,000 wa simu yako au muda wa simu nyingine. Huu ndio mpangilio wa kufuatwa:
 • Nenda kwa ‘Buy airtime’ kwa orodha yako ya M-PESA
 • Ingiza nambari ya simu ambayounanunulia muda wa maongezi.
 • Ingiza kiasi cha pesa
 • Ingiza nambari yako ya siri ya M-PESA kasha udhibitishe. Ujumbe huu utakuonyesha vile ulivyojaza, iwapo kila kitu kiko shwari bonyeza OK.
 • Utapokea ujumbe kutoka Mpesa wa kuonyesha muda wa maongezi umenunuliwa.
Kulipia bili
Wateja wa Mpesa waliosajiliwa wanaweza kulipia services walizozopata kupitia kampini zilizona mkataba na Mpesa. Baadhi ni kama kampuni ya umeme KPLC, kampini ya maji na huduma za simu. Unapolipia huduma kiwango cha juu zaidi ni Ksh. 70,000 na kiwango cha juu zaidi unachoweza kutuma ni Ksh 35,000. Kulipia huduma ni lazima;
 • Chagua ‘lipia huduma’ katika orodha ya Mpesa
 • Andika nambari ya biashara ya kampuni unayoilipa. Kampuni zinazoshiriki zina nambari spesheli za biashara.
 • Weka nambari ya akaunti ya huduma unayotaka kulipia
 • Andika kiwango cha pesa unacholipa( kati ya Ksh 100- Ksh 35,000)
 • Weka nambari yako ya siri ya Mpesa.
 • Thibitisha uliyoandika ni sawa kisha bonyeza OK.
Kutuma pesa kimataifa ukutumia M-Pesa
Waweza kupokea fedha kupitia mpango wa kimataifa wa M-pesa kutoka kwa mtu anayeishi ng’ambo. Usafirishaji huu ni wa papo hapo. Anayetuma na anayetumiwa hupokea ujumbe kutoka kwa Mpesa. Huduma hii kwa sasa iko baina ya Kenya na Uingereza. Wanaoishi UK wanaweza wakatuma fedha kupitia kwa nambari za safaricom za wanaowatumia; Western Union, Provident Capital na KenTV.
2.5
Average: 2.5 (2 votes)
Your rating: None

services provided M-pesa enough to help obat keputihan gatal and jas hujan axio yogya in managing finances.

»