Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Western Union

Nitampataje ejenti wa Western Union Kenya?

Waweza kupata ejenti wa Western Union aliye karibu na wewe kwa kutembelea ukurasa wa western union Kenya katika mtandao.

Kutuma
Ni sharti uwe na yafuatayo unapomtembelea ejenti wa Western Union;
  • Jina la unayemtumia pesa
  • Kiwango cha pesa unachotuma
  • Jiji ama nchi ambayo pesa hizo zitapokelewa.
Ukiwa huko, utapewa fomu ya kutuma ili uijaze. Ijaze kisha umkabidhi ejenti pamoja na kitambulisho, pesa unazotaka kutuma na ada ya kutuma. Ada ya kutuma huambatana na kiasi unachotuma. Ejenti atakuuliza upeane swali ambalo mpokezi ataulizwa atakapokuwa anazipokea pesa.
 
Nchini Kenya, kiwango cha juu zaidi ambacho kinaweza kutumwa ni $10,000 au Ksh. 750,000. Utapewa risiti iliyo na nambari ya Money Transfer. Kwa kutumia hiyo nambari, unaweza ukaangalia vile pesa ulizotuma zinaendelea. Mpe mtu unayemtumia pesa nambari hiyo kwa sababu inahitajika mtu anapoenda kuzichukua pesa.
 
Kupokea
Mpokezi anaweza kuchukua  pesa zake muda mfupi baada ya kutumiwa kutoka kwa ejenti yoyote aliye jijini ambalo zimetumwa. Ni lazima ajaze fomu ya kupokea, aonyeshe kitambulisho cha kitaifa, nambari ya Money Transfer (MTCN) kisha ajibu swali atakaloulizwa kikamilifu. Ni lazima uwe na miaka 18 na zaidi kupokea pesa kutoka Western Union.  
0
No votes yet
Your rating: None