Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

MoneyGram

Nitampataje ejenti wa MoneyGram nchini Kenya?

Benki za National na Co-operative ambazo zina matawi nchini kote ni maajenti wa MoneyGram nchini Kenya.  
 
Kutuma :
Tembelea ejenti wa MoneyGram na uwe na kitambulisho cha kitaifa. Jaza fomu ya kutuma kisha upeane pamoja na pesa unazotaka kutuma na ada ya kutuma. Pia waweza ukaweka ujumbe usiotozwa malipo wa maneno kumi umfikie unayemtumia pesa. Utapewa nambari ya kufuatilia. Mfikie unayemtumia pesa labda kwa njia ya simu kisha umpatie hiyo nambari. Mpokezi anaweza kupokea pesa hizo kwa dakika kumi.
 
Iwapo unatuma pesa ng’ambo, pesa zako zitabadilishwa kwa vipimo vya wakati huo vya soko la ubadilishanaji wa fedha vilivyowekwa na MoneyGram ama maejenti wake.  
 
Kupokea :
Muulize anayekutumia pesa akupe nambari aliyopewa alipokuwa anazituma pesa, hii itarahisisha upokezi. Mtembelee ejenti wa MoneyGram ukiwa na ainana kitambulisho na nambari yako. Jaza fomu ya kupokea kisha uonyeshe kitambulisho chako, utapewa pesa zako kwa sarafu za nchi yako.
0
No votes yet
Your rating: None