Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kufananisha Kati ya Kuweka akiba na Kuwekeza

Kuna tofauti kati ya kuweka akiba na kuwezeka pesa.
 
Katika kuwekeza, unajaribu kuongezea shillingi zako. Katika kuwekeza unahatarisha pesa zako lakini yawezekana ukatengeneza pesa nyingi baadaye. Huu ni uamuzi mzuri wa malengo yako ya muda mrefu.
 
Kuwekeza:
  • Kunatumika kwa malengo ya muda mrefu.
  • Unatumia pesa ukitarajia kutengeneza faida
  • Unahatarisha pesa lakini unaweza tengeneza pesa nyingi.
 
Kwa upande mwingine, kuweka akiba hakuna hatari yoyote lakini inachukua muda mrefu kwa pesa zako kupata mazao. Kwa hivyo hii ni njia nzuri ya kuhifadhi pesa za kutumia wakati wa dharura au kwa ajili ya malengo ya muda mfupi.
 
Kuweka akiba:
  • Kunatumika na malengo ya muda mfupi.
  • Unapata mazao ya chini (Pesa zako zinakua polepole)
  • Hakuna kuhatarisha pesa zako kama katika kuwekeza.
 
 
 
 

 

0
No votes yet
Your rating: None