Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Ni Nani anaweza kukusaidia?

Usiogope hatua za kuanza kuwekeza. Kuna usaidizi mwingi. Ukichagua kujaribu bila usaidizi wa mtaalam, fanya utafiti. Mtandao wa Inteneti una tovuti kadhaa zilizo na mawaidha.
 
Ukifanya pekee yako:
Kuna habari ya bure kwa mtandao ya kukusaidia kuanza. Fanya utafiti. Hii itakusaidia uwe mwekezaji hodari. Kiini cha kuwekeza ni kujua ukweli. Unaweza pata habari pia kutoka kwa maktaba za umma, duka la vitabu au magazeti. Pia unaweza kujifunza zaidi kihusu pesa katika majarida na na magazeti.
 
Jiunge na kilabu cha uwekezaji:
Unaweza elimika na pia utafurahia kuwekeza kama kikundi. Mnaweza kuwekeza pesa zenu kama kikundi na mtatoa maamuzi kuhusu pesa zenu kama kikundi. Kawaida kuna ada kila mwezi ya kushiriki kwa kilabu.Kilabu ni nzuri wa kujifundisha kuhusu uwekezaji na yaenda mkatoa uamuzi wa kustaajabisha kama kikundi.
 
Fanya kazi na dalali wa hisa:
Chaguo lingine ni kufanya kazi na mtaalam. Dalali wa hisa wana cheti cha kununulia na kuuzia watu wengine kwa soko la hisa. Wanaweza kukueleza jinsi soko la hisa hufanya kazi na wanaweza kukusaidia kuchagua uwekezaji unoakufaa kulingana na malengo yako ya muda mrefu. Unaponunua au kuuza hisa, dalali wako anapata kiasi kidogo cha bei.. Hii inaitwa Komesheni.
 
Enda darasani:
Tafuta chuo kinachofundisha kuhusu uwekezaji na jinsi ya kutumia pesa zako. Unaweza pia pata mafunzo kwa mtandao.
 
 
 
 

0
No votes yet
Your rating: None