Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Uraia Mwema

Neno uraia linamaanisha kuwa mmoja wa na kusaidia jamii na nchi yako. Kwa  kusema ‘jamii yako’ hili halimaanishi kabila lako bali watu wote ambao unaishi nao na kuingiliana nao kila siku. Uraia bora unamaanisha ya kwamba unaheshimu na kuthamini nchi yako kwa njia ambayo uko tayari kujitolea mhanga kwa ajili ya kuendelea kudumu kwake.

Ili uweze kuitwa Mkenya, una haki na ni lazima umiliki stakabadhi za usajili zinazoonyesha ya kwamba wewe ni mwananchi. Stakabadhi hizi ni kama:

 • Cheti cha kuzaliwa
 • Kitambulisho cha kitaifa
 • Pasipoti
 • PIN au nambari ya ulipaji kodi.
 • Cheti cha ndoa

Kama Mkenya, umepewa haki, fadhila na manufaa ya uraia na katiba. Katiba Mpya ya Kenya iliyoanza kutumika mnamo tarehe 27 mwezi wa Agosti mwaka wa 2010 iko na kitengo cha Haki za Binadamu kilicho bayana. Sheria ya Haki za Binadamu ni orodha ya haki za msingi za binadamu ambazo serikali ya Kenya imelazimishwa na sheria kuhakikishia wananchi wake. Hakikisha ya kwamba unaelewa haki zako kwa kusoma sura ya 4 ya Katiba Mpya ya Kenya.

Hata hivyo, haki na uhuru wa wananchi pia hukuja na majukumu. Hili linamaanisha ya kwamba unahitajika:

 • Kupata elimu
 • Kufanya kazi
 • Kulipa ushuru
 • Kupiga kura
 • Kulinda na kuhifadhi maliasili na mali ya umma
 • Kuishi kwa amani na wenzako
 • Kukuza na kutunza maisha ya familia
 • Kushiriki katika shughuli zinazochangia manufaa ya pamoja kwa Wakenya wote.

Katika sehemu hii, jifunze jinsi unaweza kuwa mwananchi anayewajibika na jinsi unaweza kunufaika kutokana na haki za kuwa Mkenya.