Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Hisa

Hisa ni sehemu ya kampuni ambayo unaweza kumiliki. Kuuza hisa kunawezesha kampuni kuunda pesa za kulipia vitu kama ujengaji wa viwanda vipya au kuajiri wafanyikazi zaidi kama njia ya kukua.

Bila hisa, kampuni kama Kenya Breweries ingekuwa kibanda kidogo katika kichochoro cha mji mdogo. Inachukua pesa kutoka kwa wawekezaji, watu wanaonunua hisa, kwa kapuni kujenga biashara yake. Watu wakinunua sehemu hizi, kampuni inapatata pesa.

Ni kweli katika historia, kuna wakati hisa zinaangamia. Wakati kampuni inafilisika au soko la hisa linaenda chini, thamani ya hisa za kampuni inateremka na muwekezaji anapata hasara. Hii ndio sababu kuwekeza kuna hatarisha pesa zako kuliko kuweka akiba.

Hisa zafanya kazi vipi?

  1. Soko la Hisa: Soko la Hisa au ‘Ubadilishaji’ ni mahali maalum ambapo wawekezaji wananununa ama kuuza hisa. Ifikirie kama soko kubwa la mitumba, pale watu wanapatana bei ya kuuza na kununua bidhaa. Hakuna bei maalum lakini vitu vinaweza kugharimu bei ya juu au ya chini kulingana na siku tofauti. Soko la hisa ni kama mnada. Ikiwa watu watapendezwa na vile hisa fulani inauza, wengi watataka kununua na bei inaweza kuongezeka, ikiwa watu hawatafurahia vile hisa inaenda, watauza na bei itaenda chini. Hivyo basi ni lazima upange kuwekeza muda mrefu na uhakikishe hakuna kununua au kuuza bila mpango.
  2. Madalali wa hisa/Wapangaji wa Fedha: Chaguo moja ni kuajiri Mpangaji wa fedha aliehitimu ama dalali mjuzi wa hisa - mtu aliyefuzwa kutunza pesa za watu. Huyu mtu ataenda sokoni kufanya biashara na kutunza pesa zako kwa niaba yako. Unapouza au kununua hisa, dalali wako anapatiwa kiwango fulani cha bei. Kiasi hiki kinajulikana kama komesheni. Sio kila mtu anayeweza kununua au kuuza katika soko la hisa. Unahitaji mtaalam ambaye ameruhusiwa kukusimamia.
  3. Kuwekeza kupitia mtandao: Hii ni njia nyingine unaweza kutumia. Unaweza kufungulia akaunti yako mtandao kuuza au kununua bila kupitia yeyote. Utahitajika kufanya utafiti ni chaguo lipi bora halafu uanze kufanya biashara bila usaidizi wa mtaalam. Watu wengine hutunza sehemu fulani ya uwekezaji wao hivi na sehemu nyingine wanajiri dalali mtaam. namna hiinkatika uchaguzi wako na uuze bila usaidizi kutoka kwa mtaalam.
  4. Kununua na kuuza Hisa: Ili ununue au uuze hisa, inahitajika kuchukua hatua chache. Ikiwa unafanya kazi na dalali, atanunua ama auze hisa kwa akaunti yako na atakwambia kama biashara iliweka faida ama hasara.
0
No votes yet
Your rating: None