Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Ufugaji Wa Mbuzi Wa Maziwa

Goats

Kwa nini nifuge mbuzi wa maziwa?
Wengi wetu hula vyakula vingi vilivyo na cabohydrates na kiwango kidogo cha vyakula vyenye madini ya protein, mafuta na vitamin. Lakini je wajua kuwa maziwa huwa na madini haya yote muhimu. Ngombe ndio tegemeo kubwa la maziwa lakini gharama na mahitaji ya kufuga ng’ombe ni ghali mno na hivyo basi njia nyingine ya kupata maziwa ni kupitia kufuga mbuzi wa maziwa. Ufugaji wa mbuzi wa maziwa ulianza maajuzi nchini lakini unaendelea kuwa maarufu.

Manufaa ya kufuga mbuzi wa maziwa badala ya ng’ombe ni kama vile:

  • Mbuzi huhitaji eneo dogo la kuwafuga ikilinganishwa na ng’ombe
  • Mbuzi hula kiwango kidogo cha chakula na maji kuliko ng’ombe
  • Kwa wale mbuzi wanaofugwa ndani ya nyumba au zero grazing, kinyesi chao huwa kikavu hivyo kurahisisha usafishaji wa chumba
  • Ni rahisi kujenga Nyumba za kufuga mbuzi kwa njia ya zero grazing na haigharimu pesa nyingi
  • Kwa jumla ufagaji wa mbuzi wa maziwa hugharimu pesa kidogo kuliko ngombe wa maziwa
  • Utapata maziwa mengi yenye madini muhimu kwa matumizi ya jamii kutokana na kiwango kidogo cha pesa ulizowekeza kwenye mradi wa kufuga mbuzi
  • Wataalamu wa lishe hushauri utumiaji wa maziwa ya mbuzi kwa sababu yana viungo muhimu mwilini .Hospitali pia huwashauri wagonjwa wanaougua Ukimwi kutumia maziwa ya mbuzi.
  • Katika maeneo ambayo watu huthamini maziwa ya mbuzi ,maziwa haya yana bei nzuri kwa mfugaji ambapo huuzwa kati ya shilingi 90 hadi shilingi 120 kwa lita moja ya maziwa
  • Ikiwa mbuzi watatunzwa vyema huwa hawachafui mazingira na ni rahisi kuwafanyia zero grazing na kuwalisha kwa majani,mimea huku kinyesi chao kinachopendwa na wakulima kikitumiwa kama mbolea shambani.
Ufugaji wa mbuzi ni mzuri haswa kwa walio na eneo dogo la shamba.
5
Average: 5 (1 vote)
Your rating: None