Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kuchagua baina ya konndoo na mbuzi

 

Chaguo la aidha kufuga kondoo ama mbuzi litategemea mapendeleo ya kibinafsi na utamaduni na kilichotayari katika sehemu yako.Barani Afrika mbuzi hufugwa kwa sababu ya maziwa na nyama ilhali kondoo wanafugwa kwa sababu ya nyama ingawaje kuna vizazi ambavyo vinaweza kukamuliwa.Maziwa ya mbuzi yanasagika kwa urahisi na ni mazuri kwa watoto wadogo,wazee na wagonjwa.Hii ni kwa sababu mafuta yamesambazika katika matone madogo madogo kote katika maziwa hivyo kuyafanya rahisi kusagika ukilinganisha na maziwa ya wenyama wengine wanaocheua.Nyama yake pia haina mafuta mengi na kwa hivyo ni rahisi kusagwa.Licha ya ugumu wao,mbuzi hawapendi kunyeshewa na kupatwa na baridi.Huathirika pakubwa na ugonjwa wa Nimonia,labda hata  zaidi ya kondoo na inaweza kuwa chanzo kikubwa cha vifo katika kundi.

 

 

5
Average: 5 (1 vote)
Your rating: None