Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Usimamizi

 

Usimamizi unajumulisha kila kitengo kilicho katika ufugaji wa wanyama ikiwemo lishe yao,uzazi,afya,makao na utunzaji wa wanyama .

Ulishaji bila  ya vikwazo

Kuchungwa na mchungaji

Kulisha kwa kufunga kamba

Kuwaletea wanyama waliofungiwa lishe

Ulishaji bila ya vikwazo

Ikiwa  kuna ardhi ya kutosha,ulishaji bila vikwazo humruhusu mnyama kuchagua na kula chakula kizuri kinachopatikana.Wanaweza kuchagua mimea iliyo mitamu,na chakula wanachokula kinategemea muda  waliopewa  machungani.Wanyama  huachwa nje ya vibanda  vyao asubuhi na hufungiwa jioni.Kasoro ya ulishaji bila vikwazo ni ya kwamba wanyama  wanaweza kula mimea ambayo hawakufaa kula  kwa mfano miti inayokua na mboga za jirani.Wanyama wanaopewa ulishaji wa   bure huibiwa kwa urahisi,huuliwa barabarani na hata huliwa na wanyama wanaowinda na kula nyama,kwa hivyo hasara inaweza kuwa juu.

Kuchungwa na  mchungaji

Hii husisha mtu ambaye huwalinda wanyama wanapokuwa machungani.Hili linaweza kuwa tatizo mahali shughuli zingine kama ukulima na majukumu ya nyumbani yanafaa kufanyika.Hili linaweza kutatuliwa na majirani wakitengeneza vikundi na kufanya zamu katika kulisha wanyama wao ili kwa njia hii ni mtu mmoja pekee  yake anayewachunga wanyama.Ulishaji unafaa kufanywa kwa mda wa masaa  manane ili kuwawezesha  wanyama  kupata lishe ya kutosha.

Kulisha kwa  kufunga kamba

Hii huhitaji jitihada ndogo kutoka kwa mkulima.Wanyama wanafaa kufungwa katika sehemu zenye chakula ama nyasi kavu na wanafaa kuhamishwa mara mbili ama tatu kwa siku ili wapate mimea ya kutosha ya kuchagua na kula.

Kuwaletea wanyama waliofungiwa lishe

Hii hujulikana pia kama ‘kata-na-beba’,mfumo unachosha kwani chakula kibivu cha kutosha kinafaa kukatwa na kubebwa kila siku ili kutoa kadiri inayofaa  ya  lishe inayotumika.Masalio ya nyumba yanaweza  pia kulishwa katika mfumo huu.Mfumo huu unahitaji usimamizi wa hali ya juu ili kuhakikisha wanyama ni wasafi,wamepata lishe na maji ya kutosha na pia uangalifu wa makini katika  uzazi na magonjwa.Kuweka wanyama kwa sakafu zilizotengenezwa na  mbao,ambao ni mtindo unaofaa huwaruhusu kubakia wakavu na  wasafi na hii hupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizo ya minyoo.Mfumo huu pia huzuia hasara kwa wizi na wanyama wawindaji. 

 

 

0
No votes yet
Your rating: None