Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Uzazi

Rika  ambayo kondoo  na mbuzi huwa tayari kujamiana hutegemea kizazi na kiwango chao cha lishe na  kwa hivyo uzani wa mwili na hali. Wana mbuzi na kondoo walio kwenye hali njema wanaweza saa zingine kufika rika ya kubalehe mapema kama hata miezi mitatu ama minne. Ikiwa hawajahanithishwa,ndume wanafaa kutengwa na kike kabla ya huu wakati ili kuzuia kujamiana masema na  kuwadhoofisha. Manii katika hiki kipindi hayawezi kua kama kawaida.

Mbuzi wa kike walio katika hali njema wanaweza kubalehe baada ya miezi mitatu (miezi tisa kwa kondoo wa kike) lakini lishe mbovu itachelewesha kubalehe. Jike hawafai kujamiana hadi wawe wakubwa kimwili na waweze kuhimili uja uzito na malezi ya wana. Wakijamiana wangali wadogo jike hamei na watoto huwa wadogo na huwa uwezekano mdogo wa kuishi. Anaweza kupata ugumu wa kupata uja uzito tena. Ulishaji mzuri ni muhimu katika kipindi cha uja  uzito haswa katika wiki chache za mwisho na mwanzoni mwa unyonyeshaji ili kuhakikisha watoto wana afya na nguvu na maziwa ni mengi kwao.  

 

 

3
Average: 3 (1 vote)
Your rating: None

nimefurahishwa na toviti
hili kwa sisi wakulima na wajasiliamali linatusaidia sana

»

Asante sana Mwajuma kwa ujumbe wako. Zidi kuipekua tovuti ya Beehive na utapata mengi zaidi. Je, kunayoyote ungetaka kujuzwa kuhusu ukulima?

»