Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Makaazi

 

Aina ya makaazi yanayohitajika yatategemea aina ya mfumo wa usimamizi uliowekewa wanyama.Mahali makundi hulishwa wakati wa mchana,na makaazi ya wakati wa usiku ambayo hutoa ulinzi dhidi ya hali ya anga na wanyama wanaowinda na kula nyama yanafaa kutolewa.Mifumo mingine huhitaji kiwango  cha juu cha ujenzi na usimamizi.

Makaazi yote yanafaa kupitisha hewa vizuri,na yanafaa kuwa na mwangaza wa kutosha,yapitishe maji vizuri na kusafishwa kwa urahisi.Zifuatazo nipointi muhimu katika utoaji wa makaazi:

Viwanja vinafaa kupitisha maji vizuri,yani havifai kufurika kunaponyesha.

Sakafu zinafaa kuwekwa kavu na kupitisha maji vizuri.Malazi yanafaa kuwa ya majani makavu ama taka taka za mbao.

Sakafu zilizoinuliwa za mbao ama saruji zinafaa kujengwa ili mianya iwe na udogo wa kutosha kuzuia kukwama kwa miguu ya wanyama wadogo.

Nyenzo za nyumbani za ujenzi,haswa wa paa zinapendekezwa.Paa  za mabati ingawaje huruhusu kukusanywa kwa maji ya  mvua,hufanya joto jingi chini yake. 

Mbuzi watatafuna nyenzo za makaazi,mbao yoyote iliyotumiwa haifai kuwa na kitu chochote cha kemikali haswa zile zinazopatikana kwenye rangi.

Makaazi yanafaa kusafishwa mara kwa mara ili kuepuka kujazana kwa samadi na magonjwa na vimelea vinavyoambatana nayo

Kujazana husababisha udhalimu na afya mbovu,makaazi yanafaa kuwa na ukubwa wa kutosha ili kuwatosheleza wanyama wote.

 

 

0
No votes yet
Your rating: None