Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Rekodi

Farmer

Rekodi Ni Nini?
Rekodi ni habari zilizokusanywa kwa mpango na kuhifadhiwa kwa uangalifu kwa minajili ya matumizi.ili kufaulu katika uendeshaji wa biashara ni lazima uwe na rekodi zilizoandikwa na kuhifadhiwa vyema. Kwa minajili na kufanya maamizi katika biashara ni lazima uweke rekodi zinazoguzia kila kitu katika biashara yako.

Rekodi zita:

  • Weza kutumiwa kukadiria faida ya mbinu tofauti za uzalishaji
  • Weza kutumiwa kulinganisha ubora wa matumizi wa rasilimali kama ardhi,leba na pesa zinazotumiwa kuanzisha biashara na njia nyinginezo za uzalishaji.
  • Husaidia mwekezaji kuboresha operesheni za shambani.
  • Hutumiwa kuhifadhi mambo muhimu ya biashara yatakayotumiwa katika siku za usoni.

Rekodi zinapaswa kutumiwa kufanya maamuzi shambani na zinafaa kutafsiriwa kwa njia mwafaka, au litakuwa ni kupoteza wakati, pesa na nguvu. Mara kwa mara rekodi huhifadhiwa kwa madhumuni kuripoti rasmi kwa mfano makao makuu ya wizara kuhusu wadudu waharibu na sio kutumiwa kama chombo kwenye shamba cha kufanya maamuzi kwa wakati unaofaa.Akili ya kuweza kukumbuka mambo ni yamanufaa lakini haiwezi kutegemewa wakati wote. Habari huweza kukumbukwa na kusahaurika.

Uwekaji wa rekodi ulio sahihi ni chombo cha maana kutathamini matokeo ya mifugo yako ili kufanya maamuzi mema.

  • Rekodi zote, inafaa kuwepo na nafasi ya maoni kueleza sababu ya kutokea kwa mambo yasiyo ya kawaida.
  • Hii ni muhimu katika kutafsiri umuhimu wa rekodi hizi kwa mtu ambaye labda hajakuwa akihusika na rekodi lakini anahitaji kufanya maamuzi ya kihakika.

 

0
No votes yet
Your rating: None