Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Vizazi Vya Ngo'mbe

Neno kizazi linamaanisha aina ya mnyama anayetambulika kutotakana na asili yake au tabia zinazomtenganisha na wanyama wengine kama rangi, umbo la mwili na ukubwa. Katika bara la Afrika kuna aina mbili kuu za ng’ombe: Wale wenye nundu (kama Boran, Sahiwal na Zebu) na vizazi vya kutoka Ulaya (kama Friesian, Jersey, Guernsey na Hereford) 

Aina hizi mbili za vizazi vya ng'ombe hufanyiwa uzalishaji ili kutoa aina ya ng’ombe ambao wanatoa maziwa na nyama zaidi na wanaweza kuhimili magonjwa ya hapa nchini. Hii iinafaa kufanyika kwa uangalifu na kwa kutafuta ushauri wa mtaalam wa uzalishaji wa ng'ombe ili upate habari zote kuhusu utunzi na mahitaji ya vizazi kutoka Ulaya.
 
Kwa upande wa kushoto, utaona viunganishi vitakavyo kuelekeza pale utajifunza zaidi kuhusu vizazi tofauti vya ng'ombe. 

 

 

1
Average: 1 (1 vote)
Your rating: None