Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kuvuna asali na nta

 Asali huvunwa mwisho wa msimu wa maua.Mfugaji wa nyuki huchagua masega  yenye asali iliyokomaa ,iliyofunikwa na rusu laini ya nta.Sega linaweza kukatwa katika vipande na kuuzwa kama sega bichi la asali,ama kuvunjwa na kuchungwa na kichungi kutenganisha asali kutoka kwa nta.  

Sega ambalo nyuki hutengeneza kiota limetengenezwa kwa nta na linaweza kuuzwa.Nta inaweza kuhifadhiwa hadi ya kutosha imekusanywa kuyeyuka juu ya maji kutengeneza pande kubwa.Wafugaji wengi wa nyuki hutupa lnta bila kujua,thamani yake.Inaweza kutumiwa kama njia ya kuzuia maji kupita na kuimarisha ngozi na pamba,katika batiki,kutengeneza mishumaa na katika mafuta kadhaa ya nywele na krimu za ngozi. Mingi ya nta kwenye soko la dunia hutolewa Afrika    

Vifaa

Vingi vya vifaa vinavyohitajika kwa ufugaji mdogo wa nyuki vinaweza kutengenezwa na mafundi vijijini.

Smoker

Mfugaji wa nyuki anahitaji chanzo tulivu cha moshi kuwatuliza nyuki anapovuna asali.moshi huu hutengenezwa na  smoka.Smoka ina sanduku la chanzo cha kawi lenye kinyesi cha ng’ombe kinachoungua polepole,kadibodi,lenye viriba.Mfugaji wa nyuki hutumia smoka karibu na lango la mzinga kabla ya kufunguliwa,na polepole huziwekea nyuki moshi ili ziondoke kutoka sehemu moja ya mzinga hadi nyingine.

Smoka 

Nyuki hukabiliana na moshi kwa kujaza asali kwa hivyo kupunguza uwezekano wao wa kung’ata.

Sanduku la chuma lina faneli yenye mwelekeo iliyotegemea juu,hivyo kuruhusu chanzo cha kawi kuingizwa ndani.

Chanzo cha kawi huwekwa sehemu ya chini na rafu ya chuma yenye matundu juu ya shimo la hewa. 

Viriba,vilivyo katika sehemu ya kulia,hutumiwa kupulizia hewa hadi kwenye sanduku la moto kupitia mashimo yaliyo mkabala.

Ni muhimu moshi tuu na sio moto unatoka kenye smoka na moto unafaa kuzimwa pindi tuu unapomaliziwa kutumiwa.

Nguo za kujikinga 

Nguo za kujikinga zinahitajika katika ufugaji wa nyuki ili kuepuka kung’atwa na nyuki,ambako kunaweza kusababisha majeraha machungu.Sehemu ya mwili iliyo muhimu zadi kuikinga ni uso,haswa macho na mdomo;Kofia ya neti yenye ukingo mpana itafanya hili. Nguo zingine zinaweza kuvaliwa,zikiwemo glovu,viatu na surupwenye.Nguo nyeupe zinashauriwa ,kwani nyuki wana uwezekano mkubwa wa kung’ata nguo nyeusi. Chochote unachovaa,hakikisha nguo haziko wazi na nyuki haziwezi kupitia kwani hii inaweza kuwa chungu. 

Vyombo vya mzinga  

Chombo cha mzinga ni kipande cha chuma kinachotumiwa kufungua masanduku,kugwaruza vipande vya nta,kutenganisha fremu kutoka kwa vitegemezi na kadhalika.Vinaweza kutengenezwa kutoka kwa vipande tambarare vya chuma cha pua;bisibisi mara  kwa mara hutumiwa.Visu vizee vinaweza kutumiwa lakini hunyumbulika na havitoi nguvu ya wenzo ya kutosha. 

 

0
No votes yet
Your rating: None