Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Mazao kutoka kwa ufugaji wa nyuki

Ufugaji wa nyuki huzalisha mazao mengi ya msingi lakini yale yanayotambulika sana ni asali na nta,lakini chavua,propolisi,jeli,sumu,malkia,nyuki na viluwiluwi ni mazao ya nyuki ya msingi yanayoweza kuuzwa.Ingawaje mengi ya mazao haya yanaweza kutumika au kuliwa jinsi yalivyotolewa na nyuki,kuna matumizi mengi ya ziada ambayo bidhaa hizi hutengeneza sehemu ama kiambato cha bidhaa zingine.Mingi ya mazao ya msingi ya ufugaji wa nyuki hayana soko hadi yaongozwe kwenye thamani ya bidhaa zinazotumika kwa wingi.Hata thamani ya bidhaa za msingi inaweza kuongezeka ikiwa utumizi mzuri utafanywa kwenye bidhaa zingine,hiyo kuongeza faida kwa mingi za shughuli za ufugaji wa nyuki.       

Asali:

Asali hutumiwa kama chakula,kiambato cha chakula,dawa,na katika kiwanda cha tumbaku kuboresha na kuhifadhi harufu na unyevu,katika vipodozi kama matibabu ya ngozi,kuhifadhi maji na,kulainisha ngozi na katika krimu,sabuni,shampuu na rangi za mdomo.  

Chavua

Chavua hutumika kama chakula,dawa na vipodozi 

Nta

Hutumiawa katika utengeaneazaji wa mishumaa,vipodozi,kutengeneza vyakula,nguo,katika vanishi na polishi,upigaji chapa,katika dawa na kufinyanga na kuchonga vinyago

Propolisi 

Propolisi ni mchanganyiko wa nta ya nyuki na utomvu unaokusanywa na nyuki anayetengeneza asali kutoka kwa mimea haswa maua na kichomoza cha jani.

Nyuki hutumia propolisi kulainisha kiota na masega na kurekebisha nyufa ndani ya mzinga.

Propolisi hutumiwa katika vipodozi,dawa na katika teknolojia ya vyakula.

Jeli ya kifalme:(hiki ni kitu  chenye wingi wa madini ya protini ambacho nyuki wafanya kazi hutumia kulisha viluwiluwi  katika kipindi cha awali cha kukua na viluwiluwi vya nyuki malkia katika vipindi vyao vyote vya kukua)

Nyuki wafanyakazi wachanga ndio hutoa jeli ya kifalme ili kulisha viluwiluwi wachanga na nyuki malkia aliyekomaa.Jeli ya kifalme hutumiwa kama nyongeza kwa vyakula,na kama kiambato katika bidhaa za vyakula,dawa,vipodozi na kwa lishe ya wanyama. 

Sumu

Nyuki  hutoa sumu wanapouma kama njia ya kujilinda.Sumu ya nyuki hutumiwa kama dawa kutibu mzio unao sababishwa na kuumwa kwa nyuki.

 

 

 

 

 

 

0
No votes yet
Your rating: None