Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Ufugaji wa nyuki kama shughuli muhimu

Ufugaji wa nyuki ni shughuli,inayowiiana vyema na miradi mingine ya maendeleo ya ukulima na mashambani.Miradi ya maendeleo katika maeneo pia hutoa uwezekano kwa utekelezaji wa ufugaji wa nyuki.  

Mimea fulani ikipandwa katika miradi Kama hii inaweza kuzalisha asali kwa mfugaji wa nyuki vile vile kunufaika kutoka kwa shughuli za uchavushaji za nyuki.Ufugaji wa nyuki unaweza kumtolea kipato cha ziada mkulima mdogo anayepanda mimea hii ama ana nyuki karibu. 

Mimea ifuatayo inajulikana kwa kuwa ya manufaa kwa uchavushaji wa wadudu.Ile iliyowekwa alama ya nyota pia ni vyanzo vizuri vya mbochi kwa nyuki wanaotoa asali.

Mkonge,korosho,chai,paipai,nazi,kahawa,boga,tango,mawese,lichi,mchungwa/mdimu/mlimau,tufaha,parachichi,klova,tikitimaji,mpichi,mberimweusi ufuta,alizeti,maharagwe ya soya(baadhi ya aina) na alfalfa.

Mimea hunufaika kutoka kwa uchavushaji wa wadudu kwa ongozeko la seti ya mbegu.Hii husababisha ongezeko la mbegu na matunda  ya hali ya juu.Nyuki ni wa manufaa kama wachavushaji katika hizo sehemu ambazo wadudu halisi wa uchavushaji hawapatikani ama hawatoshi kuchavusha sehemu kubwa  zilizotengewa mmea mmoja.(kumbuka hata hivyo nyuki hawavutiwi na mimea yote) 

Watu wanaojihusisha na na miradi ya misitu huwa wanavutiwa sana na ufugaji wa nyuki.Ufugaji wa nyuki ni kazi inayoleta  mapato ikiwekwa kwenye raslimali ya msiti,hata hivyo sio haribifu kwa rasilmali hiyo.Mtu anayepata  kipato kutoka kwa ufugaji wa nyuki kwa haraka anaweza kuwa mtetezi wa uhifadhi wa raslimali ya msitu.Ufugaji wa nyuki pia unapunguza uwezekano wa mto wa vichaka inayoashwa na wawindaji wa nyuki wanapochoma nyuki kutoka kwenye koloni za mbugani.   

Aina ya miti inayotumiwa katika juhudi za upandaji wa misitu ambayo ni chakula kizuri cha nyuki inaweza kuhusika katika uanzishaji wa kiwanda cha ufugaji wa nyuki.Ufugaji wa nyuki ni sehemu ya kutumia rasilmali ya msitu yenye maiumizi chungu mzima.

Miti inayotumika kwa madhumuni ya kuni,kinga ya mimea na kivuli,pia hutoa mbochi wa kutosha kuzalisha asali katika maeneo mengine.Kama ilivvyo utokaji wa mbochi hutegemea mambo mengi(tabia ya nchi(hali ya joto,baridi ,mvua n.k),hali ya anga na ardhi),mti labda hauwezi kuwa mtoaji mzuri wa mbochi unapopelekwa katika eneo jipya.Angalia ikiwa aina ya mti ni nzuri katika utoaji wa mbochi katika hali utakaokuwa ukimea kabla ya kupigania utumizi wake kama chanzo kizuri cha mbochi kwa nyuki.   

 

 

5
Average: 5 (1 vote)
Your rating: None