Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Ufugaji wa Ndege

Ufugaji wa kuku

 

Inapokuja katika ufugaji wa ndege,mbinu inayotumiwa kijijini ile ndege huachwa azurure katika boma bila uchungaji ama  na uchungaji mdogo.Kuna shida nyingi ndege huona:

1.  Ndege halishwi vyema kwani hula masalio ya.chakula,minyoo wachache na mabaki mengine wanayoyapata.   

2.  Vifaranga wadogo huachwa washindanie chakula na ndege wakubwa na huwa nyama rahisi kwa wanyama wanaowinda na kula nyama na husambaza magonjwa. 

3.  Ndege hawapati maji ya kutosha na hawana mahali pa kujisetiri idhidi ya upepo na mvua ama kuwaweka salama dhidi ya wanyama wanaowinda na kula nyama bila kusahau wezi. 

4.  Ndege hutaga mayai ardhini na yanaweza  kuharibiwa kwa urahisi na kuliwa na wanyama wengine.

5.  Sio kawaida ndege kupewa chanjo na matibabu dhidi ya magonjwa na vimelea.

Matokeo ni ndege wengi huwa wagonjwa na hukua pole pole,hutaga mayai machache na nyama kidogo.  

Ili kuhakikisha mapato mazuri kutoka kwa ndege wako,unapaswa:

1.  Kuwapatia ndege mgawo mzuri wa vyakula tofauti na maji safi.Ikitegemea wakati wa mwaka,wataweza kujitafutia chakula kwa kugwaruza ardhi katika boma. 

2.  Wapatie chakula cha ziada ili ndege waongeze uzani na kuku watage mayai mengi zaidi.

3.  Walishe vifaranga na chakula kilicho na protini kama konokono,minyoo na mchwa ili wakue kwa haraka na wawe na afya.

4.  Wajengee  kuku mahali penye giza na  patulivu ambapo wanaweza kutaga mayai yao.Kuku hutaka kusikia wakiwa salama kutoka kwa wanyama wanaowinda na kula nyama na wapita njia.

Kama ndege watasumbuliwa mara kwa mara watakuwa wakiviacha viota vyao na hii huathiri uanguaji wa mayai.

5.   Ikiwa nia yako ni utoaji wa mayai,ni vizuri kufuga kuku wa kike pekee.Jogoo mmoja anaweza kufugwa aangalie wanyama wanaowinda na kula nyama na kuwahudumia kuku.Wakati jogoo wa ziada wanapofikia umri wa kuuzwa,wanafaa kuuzwa,kuchinjwa ama kutolewa kama zawadi kuzuia jogoo kula chakula ambacho ni adimu na kupigana na kuwataabisha kuku.

6.  Ukubwa wa kundi unafaa kuafikiana na ukubwa wa nyumba,kiasi cha chakula unachoweza kununua na raslimali za chakula katika maeneo yanayokuzunguka.

7.  Usinunue ndege kutokakwa vyanzo ambavyo havijathibitiwa haswa vipindi milipuko ya magonjwa  ni kawaida kwa sababu wanaweza kusambaza magonjwa kwa wengine.

8.  Toa chanjo mara kwa mara kulingana na ushauri wa watoaji chanjo na madaktari wa wanyama wa nyumbani.

Vifaranga wachanga wanapaswa kuchanjwa dhidi ya magonjwa ya kawaida ya kuambukizana wakifika umri wa wiki 2-3.

9.  Ikiwa ndege watataabika kutoka kwa ugonjwa sugu unapaswa:

Kuita   daktari wa wanyama

Kumwtenga kutoska kwa wengine

Ndege anafaa kuuliwa mara moja kwa kutegemea jinsi ugonjwa ulivyo mzito na 

Anafaa kuchomwa ama kuzikwa katika kina kirefu ili kuzuia mbwa na wanyama wengine kuwachimba na kusambaza ugonjwa.

10.  Angalia  ni kuku wagani wana dalili za kutaka kuangua mara moja kwa mwezi na watolee 

utunzaji wa ziada.

 

 

4
Average: 4 (1 vote)
Your rating: None