Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Matibabu na chanjo

Matibabu

Magonjwa mengine yanaweza kutibiwa na dawa.Magonjwa ya vimkelea,kama chawa ma minyoo yanaweza kutibiwa na dawa zinazopambana na vimelea ama kwa kutumia mbinu rahisi kama kuosha ndani ya mafuta.Magonjwa mengine yanayosababishwa na bakteria kama kuendesha,yanaweza kutibiwa na kiua vijasumu.Kwa magonjwa ya virusi hakuna tiba.Lakini magonjwa ya virusi yanaweza kuzuiwa kwa chanjo.

Chanjo
 
Ndege wote wanafaa kuchanjwa dhidi ya magonjwa mengi ya virusi na ya kawaida katika eneo.Mipango ya utoaji wa chanjo katika daraja la kijiji inafaa kushughulikia ugonjwa wa Newcastle na ndui ya kuku.Chanjo dhidi ya homa ya ndege inafa kuepukwa ila tu kama imeidhinishwa na mamlaka ya matibabu ya wanyama.Magonjwa mengine yanayosababishwa na virusi kama ugonjwa wa Gumboro na Marek yanaweza kutolewa chanjo,lakini hayana umuhimu mkubwa vijijini.Ugonjwa unaosababishwa na bakteria kama kipindupindu cha kuku unaweza kuzuiwa na chanjo.Ndege wanafaa kuchanjwa wangali wachanga na kabla ya kuanza kutaga mayai.Ndege wengi ambao hawajachanjwa hawawezi kuhimili magonjwa na hufa.Chanjo zinafaa kutolewa tu kwa ndege walio na afya. 
 

 

0
No votes yet
Your rating: None