Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Magonjwa muhimu ya ndege

 

Magonjwa huainishwa kulingana na bayolojia yao,kama Virusi,Bakteria,Kupe,ukungu,na chanzo chao,kwa mfano magonjwa ya lishe yaliyoangaliwa hapo juu.Hata hivyo,magonjwa muhimu katika ndege yamegawanywa katika makundi matatu kulingana na makali yao na umuhimu katika mfumo wa uzalishhaji mdogo katika vijiji.Vitu muhimu kama tabia zao wakati wa mlipuko(dalili),na matibabu yanayowezekana(kuzuia ama kudhibiti)vile vile wakati wa kutokea utatolewa.Umuhimu wa ugonjwa hutathminiwa na idadi ya vifo na athari kwa uzalishaji,na itatofautiana kutoka eneo hadi eneo na msimu hadi msimu.

Mchanganyiko wa magonjwa

Magonjwa kadhaa yasiyo muhimu yanaweza kukutana na magonjwa mengine na kusababisha madhara makali kwa ndege.Hii ndio hali kwa mfano maambukizo ya E.coli, utapiamlo na kupe wa ndani.Magonjwa kama haya ni  vigumu kuua ndege lakini huwa na madhara makubwa kwa kinga ya ndege dhidi ya magonjwa,na kujenga msingi wa maambukizo rahisi ya magonjwa mengine.

Umuhimu mkubwa huashiria ugonjwa wa kawaida wenye vifo vingi(zaidi ya asilimia 30 ya kundi),husambaa kwa urahisi na ni vigumu kutibu.Umuhimu wa wastaani kawaida ,vifo vya wastani(10-30%) ya kundi na /ama vigumu kutibu.Usio muhimu hauashiria kawaida vifo vichache na /ama  rahisi  kutibu. 

Ugonjwa wa kuambukizana wa kuku unaoshambulia mapafu na mfumo wa neva

Ugonjwa huu huuwa ni wa kawaida katika msimu wa mvua,na hutokea mara kwa mara katika vifaranga wachanga,lakini pia katika kuku waliokomaa.Vifo vya juu katika kundi,mara kwa mara baina ya aslimia 30 na asilimia 80 ya ndege hufa,ugonjwa unapowakumba.Kuku hupoteza hamu ya kula na usagaji mbaya wa chakula tumboni.

Wanaweza kuonyesha upumuaji mzito,kinyesi cha kijani na saa zingine kuhara damu.

Wanaweza kuonyesha dalili za kuchanganyikiwa,kiharusi na hufa ghafla.Dalili zinaweza kutokea zote wakati mmoja.Ugonjwa huu ni wa kirusi kwa hivyo hauna tiba,lakini unaweza kuzuiwa kwa kuwachanja ndege wote ukijumuisha vifaranga wa kutoka wiki mbili.   

Homa ya ndege(AI)

Ugonjwa huu hupatikana kwa kawaida katika bata na bata wa maji,na unaweza kusambaa kama ugonjwa ambao husambaa kwa mfumo ambao ni rahisi kusambaa na ni hatari kwa kuku.Vifo vya juu katika kundi,ndevu na undu wa jogoo hufura na wenye rangi ya samawati.Husambaa kupitia chakula na maji yaliyochafuliwa kati4ka madimbwi.Ugonjwa huu ni kirusi ,kwa hivyo hauna tiba.

Kuzuia ni kuzingatia usafi na kuchinja ndege wagoinjwa.Homa ya ndege hivi sasa HAIWEZI kuzuiwa kwa kuchanja ndege.Kuua(ndege wasiohitajika ) na kuchoma ndege wote katika kundi na kuosha kwa makini nyumba ya kuku kunafaa kutiliwa maanani baada ya mlipuko wa ugonjwa.Daima muite daktari wa wanyama,ikiwa unashuku mlipuko wa homa ya ndege.Usiwale ndege walioadhirika.

Ndui ya kuku

Huonekana mara kwa mara katika vifaranga wadogo,lakini pia kwa kuku waliokomaa na huonekana kama mafumba madogo madogo kwenye ndevu,undu na uso.Hali joto ya mwili iliyo juu,uchovu unaoambatana na kifo cha ghafla.Ugonjwa huu ni wa kawaida wakati wa misimu ya kiangazi,lakini pia  unaweza kutokea mwaka mzima.Ugonjwa huu ni kirusi kwa hivyo hauna tiba.Chanjo inapatikana na ni yenye kufaa. 

Ugonjwa wa Marek

Huonekana tu katika ndege walio na zaidi ya wiki 16.Mwanzoni ndege wanaweza kuonyesha kiharusi kwa mbawa moja ama zote mbili.Ama mguu mmoja ama yote inaweza kupooza.Ugonjwa huu ni kirusi,kwa hivyo hauna tiba,lakini chanjo zinazouzwa zinapatikana.

Ambukizo la Bacteria ya E.coli

Hutokea sana sana katika vifaranga walioanguliwa,na husababisha ambukizo katika eneo la tumbo.Dalili katika ndege wakubwa:ugumu wa kupumua ama ambukizo katika sehemu ya yai na kusimama kwa utoaji wa mayai.Kuzuia kunako faa ni kuboresha usafi wa mayai ya kuanguliwa na pia kiota.Tiba kwa vifaranga wagonjwa inawezekana ukiwa na kiua vijasumu. 

Kipindupindu cha kuku(pasteurellosis) 

Unaweza kutokea wakati wowote na kwa rika zote.Dalili ni kuendesha vibaya,dalili za kupumua,kukosa hamu ya kula,ndevu na undu wa jogoo wa samawati.Unaweza kutokea kama ugonjwa sugu ama kukumbwa na kifo cha ghafla.Mambukizo kupitia chakula ama maji yaliyochafuliwa.Hauna tiba.kuzuia kuzuri ni usafi wa hali ya juu na chanjo.Ua ana uchome ndege walioathirika.Chanjo inapatikana.

Ugonjwa wa  kuhara katika ndege wachanga unaosababishwa na bacteria aina ya salmonella pullorum(Bacillary white bacteria)

Hutokea sana sana katika vifaranga wachanga.Vifaranga hutedmbea kwa ugumu,huonyesha tumbo kubwa na hukokota mbawa zao.Kinyesi chao huwa maji maji na hugeuka cheupe.Hauna tiba.Kuzuia ni kutilia usafi maanani.Ikiwa ugonjwa utatokea,tenga ama ua na uchome ndege.Ugonjwa huu husambazwa kwa kifaranga kutoka kwa mayai ya kuku aliyeathirika,ambaye haonyeshi daalili zozote za kuwa mgonjwa.

Homa ya matumbo ya kuku

Huonekana zaidi kwa kuku wakubwa.Dalili:hali jioto ya mwili iliyo juu,uchovu,undu ya samawati.Hauna tiba.Kinga ni kutilia usafi maanani na kuua kuku wagonjwa.Usinunue vifaranga kutoka kwa vyanzo ambavyo hauvijui,na usitumie mayai kwa ajili ya kuanguliwa kutoka kwa kuku ambao wamekuwa wagonjwa.

Gumboro(Infectious Bursal Disease,IBD)

Huonekana tu katika vifaranga walio chini ya wiki 6,na ni wa kawaida katika makundi makubwa ambayo yamefugwa katika sehemu zilizofungwa.Sio  wa kawaida katika mfumo mdogo wa vijijini.Dalili za kawaida: Kuendesha.Ugonjwa huu ni kirusi ,kwa hivyo hauna tiba.Chanjo inapatikana.

Ugonjwa wa kupumua katika ndege 

Dalili:Pua linalotoka makamasi,mavimbe chini ya macho,macho yaliyojifunga,upungufu katika utagaji wa mayai.Tiba ni kuongeza kiua vijasumu katika maji ya kunywa. 

Ugonjwa sugu wa kupumua (Mycoplsmosis)

Dalili:Pua linalotoka makamasi ama lililozibwa,uso uliofura,macho yaliyojifunga,upungufu katika utagaji wa mayai,vifo visivyo vya kawaida.Tiba ni kuongeza kiua vijasumu katika maji ya kunywa. 

Ugonjwa unaosababisha kuendesha (kimelea cha ndani) 

Ugonjwa huu unaweza kutokea wakati wowote na katika rika zote,lakini unaweza kuzuiwa kwa kusafisha kwa makini kwa vihori na nyumba za ndege.Dalili:Kugonjeka,kuchoka,kichwa  chini ,manyoya yaliyotimka,kuhara damu.Vifo katika vifaranga wachanga.Ikiwa vifaranga wataendelea kuishi watabakia kuwa wembamba na watachelewa kutaga.Tiba:Weka dawa ya  kukabiliana na Coccidiostatics katika maji ya kunywa ama lishe.Kuzuia:Usiweke ndege wengi pamoja.Epuka kuweka ndege wa rika mbalimbali katika nyumba moja kwani ugonjwa unaweza kusambaa kutoka  kwa kuku wakubwa hadi kwa vifaranga.

Minyoo mviringo na tegu (vimelea vya ndani)

Vimelea vya ndani ni vya kawaida katika umri wote katika mfumo wa uzalishaji vijijini.Vimelea hivi husababisha afya mbovu,kupoteza uzani,kupungua kwa uzalishaji wa mayai.Tiba bora ni kuongeza dawa ya kupigana na minyoo katika maji ya kunywa mara moja ama mbili kwa mwaka,ikiwezekana wiki mbili kabla ya chanjo dhidi ya upungufu katika lishe.Usafi wa makini unaweza kuzuia ambukizo kubwa.

Vimelea vya nje

Huvamia rika  zote wakati wowote,lakini hutokea mara kwa mara katika nyumba za kuku zenye unyevunyevu na uchafu.Ndege waliokomaa husumbuliwa na hutumia wakati mwingi wakidonoa na kusugua manyoa.Vifaranga wachanga wanaweza kufa kwa sababu ya upungufu wa damu (anaemia).Kama  hautatibiwa nyerenyere,chawa,viroboto,kupe watasababisha upotezaji wa uzani na pia kuna uwezekano wa kupoteza manyoya kwa sababu ya kunyonywa damu na vimelea na kuwashwa na ngozi.Chawa wanaweza kuonekana karibu na macho na mapua.Viroboto vinaweza kuonekana kwa tumbo.Tiba:Nyunyiza  dawa ya kuua vimelea,jivu na mafuta.Jivu na poda ya salfa inaweza kutumiwa mahali ambapo kuku huoga na mchanga.Viota vinaweza kulindwa kwa kuwekewa majani kadhaa ya tumbaku yaliyochanganishwa na jivu katika viota.

Miguu yenye magamba

Miguu yenye magamba husababishwa na vimelea vya nje vinavyowasha ngozi kwenye miguu ya ndege.Dalili:Miguu ina magamba yanayoonekana na majeraha  na anaweza kulemazwa katika umbo.Tiba:Weka miguu kila siku kwenye mafuta taa,mafuta ama katika dawa ya kuua wadudu hadi magamba yatoweke.

Magonjwa yanayosababishwa na lishe

Dalili:Kuumbuka kwa mifupa na kupotea kwa manyoya.Ndege hutembea kwa ugumu;huchopea .Miguu imeumbuka.Upungufu mwingine unaoweza kusababisha kupotea kwa manyoya.Tiba,ukitambulika kwa wakati unaofaa :Vitamini nyongeza na madini ya kalshiamu,nyasi bichi na kinyesi cha ng’ombe.Magonjwa yanayosababishwa na lishe yanaweza kuzuiwa wakati ndege wanaweza kupata mimea na hayapatikani katika kuku wanaojitafutia chakula.

 

 

5
Average: 5 (1 vote)
Your rating: None