Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Tahadhari za kuchukuliwa unapotoa chanjo

 

1.Chanjo zote zinafaa kuhifadhiwa kahtika jokofu kabla ya kutumika.

2.Chanjo zingine zinazoitwa uthibiti joto,na hii ina maanisha chanjo hizi zinaweza kuhimili halisjoto kali.Hata hivyo chanjo zinazothibiti joto zinafaa kuhifadhiwa mahali patulivu ili kuzifanya ziwe na uwezo wa kufanya kazi.Unapaswa kuziweka chanjo mbali na jua la moja kwa moja. 

3.Unapotumia chanjo kiwanjani,unapaswa kwa umbali unaowezekana kuzisafirisha katika sanduku tulivu na lenye barafu.

4.Sirinji,sindano na vifaa vingine vitakavyo tumika wakati wa utoaji wa chanjo havifai kuohshwa na viua viini vya kemikali kwani vinaweza kuharibu chanjo.Badala yake vinapfaa kuuliwa viini kwa kuwekwa katika maji ya moto na hatimaye kutumiwa baada ya kupoa.  

5.Chaanjo ni lazima zichanganyishwe ama kuzimuliwa na Maji baridi yaliyotoneshwa,na tahadhari inafaa kuchukuliwa ili kuhakikisha chanjo hazipatani na jua la moja kwa moja.

6.Ni vizuri kuwachanja ndege katika masaa matulivu ya siku,aidha asubuhi ama jioni.

7.Baadhi ya chanjo zilizochanganyishwa zinafaa kuutumiwa katika mda usiozidi dakika 30.Ama hazitafaa kwa matumizi na zinafaa kutupwa.

8.Mara kwa mara tafuta ushauri wa dakitari wa wanyama ama mzaidizi wa dakitari wa wanyama kabla ya kufanya kampeni ya chanjo.

 

 

0
No votes yet
Your rating: None