Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Mbinu za kutoa chanja

 

Kuna mbinu nne za msingi za kuchanja ndege:

1.Matone ya macho

2.Sindano

3.Utoboaji wa ngozi

4.Kupitia mdomo (katika lishe ama maji)

Kwa ndege wanaojitafutia chakula,unapaswa kuepuka kuchanganyisha chanjo na maji ya kunywa ama chakula,kwa sababu ni vigumu kutoa kiwango kinachofaa.Utafiti umeonyesha ya kwamba kinga dhidi ya ugonjwa kwa mfano ugonjwa wa Newcastle hubadilika ikiwa chanjo imetolewa kupitia kwa maji ama chakula.Kutoa  kiwango kinachofaa ni muhimu kwa chanjo kufanya kazi vizuri.Kiwango cha  juu sana cha chanjo iliyo hai kinaweza kumuua kifaranga mchanga ,ilhali kiwango cha chini zaidi hakitatoa ulinzi wa kutosha.Kwa hivyo ni muhimu kutafuta ushauri wa dakitari wa wanyama madaktri wasaidizi wa wanyama (madaktari wa wanyama wanaozunguka zunguka,watoaji chanjo katika  vijiji) kwa ushauri zaidi kabla ya kutoa chanjo.

 

0
No votes yet
Your rating: None