Hapa kuna orodha ya majina yanayoweza kuwa na msaada kwako unaposoma kuhusu elimu.
Raslimali: Mali au vitu unavyomiliki ambavyo unaweza kuuza kwa minajili ya fedha.
Anayenufaika: Yule atayezipata pesa.
Dalali: Huyu mtu anayenunua au kuuza bidhaa kwa watu wa kawaida katika soko la ubadilishaji fedha madalali pia huweza kuuza bidhaa nyinginezo vinavyohusiana na mambo ya kifedha kama sera.
Mlezi/Mtunzaji: Mtu mzima anayechukua majukumu ya kuwatunza watoto wadogo (Chini ya miaka 18)
Metegemezi: Mtu anayetegemea msaada kutoka kwa wazazi au mtunzaji/walezi.
Mahali pa ubadilishaji: Mahali ambapo hisa hufanyiwa biashara
Msaada wa kifedha: Pesa zinazokusaidia kulipia masomo yako
Riba: Ada unayolipa unapokopa pesa
Ukamavu (maturity): Wakati pesa zako hulipwa na shirika
Kiwango cha ulipwaji: Pesa unazopokea kwa kipindi fulani
Elimu ya daraja ya juu: Mafunzo yajayo baada ya sekondari na chuo kikuu
Upunguzaji wa kodi: Pesa unazolipa huondolewa kwa jumla ya fedha ulizo nazo kwa ajili ya kodi
Karo: Malipo yalipwayo shuleni kwa minajili ya masomo kama chuo kikuu au taasisi nyinginezo.