Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Mipango ya kibinafsi ya malipo ya uzeeni

Iwapo umejiajiri au unafanya kazi isiyo ya ofisi labda unashangaa ni vipi utajipanga kwa kustaafu kwako. Jawabu lako ni kuchagua mojawapo ya mipango ya kibinafsi ya malipo ya uzeeni. Mipango ya kibinafsi hupeanwa sana na mashirika ya fedha kama benki na kampuni za bima. Kwa vile ni nyingi ni sharti uzingatie yafuatayo kabla ya kufanya uamuzi:
 • Hali yako ya sasa iko vipi na mipango yako ya baadaye ni ipi?
 • Kampuni hiyo ina sifa zipi? Wakurugenzi na washikadau wenginewana sifa nzuri?
 • Kampuni hiyo ina uwezo upi wa kiufundi?
 • Chunguza huduma zao kwa wateja. Je wana shughulikia kila mtu binafsi?
 • Chunguza uwezo wao wa kuweka rekodi.
 • Angalia matokeo yao ya awali ya kazi. Viini vya upungufu vilikuwa vipi iwapo kuna vyovyote?
 • Wanatoza ada kiasi kipi kwa huduma zao?
 • Ni faini ipi iliyoko iwapo mwanachama hataweza kutoa malipo kama inavyihitajika, labda kwa kupoteza kazi, ugonjwa au kupumzika kikazi?
 • Utoaji wa malipo - iwapo utoaji wa malipo huwa kiasi kimoja kwa kipindi cha miaka kadha au mtu anaweza kubadilisha kiasi cha malipo na kama kufanya hivyo kutagharimu fedha.
 • Je mwanachama anaweza kushiriki katika kuchagua uekezaji wa pesa zinazolipwa?
 • Je wana ufaidi zaidi kama mipango ya elimu. 
Hapa chini utapata mifano ya mashirika ya fedha yaliyo na matawi katika miji mingi nchini Kenya ambayo ina huduma za hazina ya kibinafsi ya kustaafu. Pia waweza tembelea benki yoyote ama kampuni ya bima kokote uliko kisha uulizie iwapo wana mpangilio huo.
 • UAP Provincial Insurance Company Limited - Individual Retirement Benefits Schemes
 • Cannon Personal Pension Plan Insurance
 • Co-op Trust Limited Individual Pension Plan Bank
 • Jubilee Insurance Company Ltd Personal Pension Plan Insurance
 • Amana Personal Pension Plan Fund Manager
 • ICEA Individual Retirement Benefits Scheme Insurance
 • Madison Insurance Personal Pension Plan Insurance 
Huu nimpango madhubuti kumaanisha kuwa waweza kubadilisha kazi bila kupoteza akiba yako ambayo pia haitozwi ushuru.

 

0
No votes yet
Your rating: None