Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Anza Kupanga Leo

Si mapema kuzingatia mipango ya kustaafu. Hakika ukiwa na umri mdogo ni bora kuanza kwa sababu utakuwa na muda zaidi wakuweka pesa zako. Yafuatayo ni vidokezo vya kukusaidia kujitayarisha kustaafu. 

  • Lipa madeni yako kwanza: Ni wazo nzuri kuwa na mipango ya kuweka akiba ya kustaafu na ikiwa umeajiriwa itakubidi uchangie malipo ya kiinua mgongo ya kampuni inayokuajiri. Njia moja ya kuhakikisha usalama wa kustaafu ni kulipa madeni makubwa, kama vile mkopo wa kununua magari, nyumba na mengineo. Kwa hivyo hautakuwa na deni wakati mapato yako yatapungua na utakuwa tayari unamiliki gari na nyumba yako.
  • Fikiria kabla ya kutumia pesa zako: Unaweza kutamani TV kubwa au gari nzuri. Lakini kwa miaka michache baadaye, hazitakuwa na thamani na utakuwa na pesa kidogo ukistaafu.  
  • Wezeka katika mipango mingi ya akiba: Kampuni yako inaweza kuwa na pensheni ya lazima lakini hii haimaanishi huwezi wekeza na mipango mingine kama vile bima ya maisha au mchango shirikisha(mutual funds). Kama unaweza kuwekeza fedha zako kwa njia tofauti, hakikisha umejenga hazina nzuri.
  • Tafuta mshauri wa fedha: Mshauri mzuri wa fedha ni yule ushauri wake una thamani kama kipande cha dhahabu. Atakusaidia kuwekeza akiba yako katika sehemu inayofaa na anaweza kukusaidia pakubwa ikiwa pesa zako zimefungika na unawasiwasi vipi unavyoweza kuinua malipo yako. Washauri wengi wa fedha wanapata mapato yao kutoka kwa kampuni zilizo waajiri. Kwa hivyo, hutalipa chochote.  
  • Zingatia utakachofanya unapostaafu: Unaweza kutumia ujuzi wako katika sehemu mbalimbali, ama unaweza kuwa na uraibu (hobby) utakaogeuka na kuwa biashara ndogo. Unaweza kutarajia kunawiri muda mrefu hata baada ya kustaafu rasmi.    

 

 

0
No votes yet
Your rating: None