Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Vikwazo kwa uzalishaji wa muhogo

Wadudu waharibifu wanaoathiri muhogo pakubwa barani Afrika ni nyenyere wa kijani wa muhogo,cassava mealybug na panzi aliyechujika.Magonjwa makuu yanayoathiri muhogo ni ugonjwa wa cassava mosaic,cassava bacterial blight,ugonjwa wa casava anthracnose na kuoza kwa mzizi.Wadudu waharibifu na magonjwa,pamoja na mbinu mbaya za ukulima huungana kusababisha kupotea kwa mazao kunakoweza kuwa wa hadi asilimia 50 barani Afrika.

Uzalishaji wa muhogo hutegemea usambazaji wa vipande vya mashina yaliyokatwa vyenye ubora wa juu.Kiasi cha ongezeko la nyenzo hizi za kupanda ni wa chini ukilinganisha na mazao ya mbegu yanayapandwa na mbegu za ukweli.Kwa kuongezea mashina yaliyokatwa ya muhogo yana ukubwa na huharibika kwa urahisi kwani hukauka katika mda wa siku chache.

Kama zao la mzizi,muhogo huhitaji kiasi kikubwa cha kazi ili kuvuna.Kwani huharibika kwa urahisi,mizizi inafaa kutengenezwa kwa njia inayoiwezesha kuhifadhiwa pindi tu inapovunwa.

Mmea wa muhogo hupandwa kwa ajili ya mizizi yake ambayo hutumiwa kama chakula.Muhogo una uwezo wa kumea katika udongo ambao mimea mingine haiwezi kumea vizuri.Muhogo pia ni mmea unaofaa kupandwa ikiwa kuna kiangazi.Kwa sababu mizizi ya mihogo inaweza kuhifadhiwa chini ya ardhi kwa mda wa hadi miezi 24 na aina zingine kwa mda wa hadi miezi 36,uvunaji unaweza kucheleweshwa hadi soko,utengenezaji na hali zingine zinafaa.

Mmea wa muhogo hutumiwa sana sana kama chakula cha kutumiwa na binadamu.Unaweza pia kutumiwa kama chakula cha wanyama.Katika nyumba mingi muhogo hutoa chanzo cha chakula na hutoa nishati.Unaweza kutengenezwa kuwa unga wa uji ama ugali ama kuchomwa ama kuchemshwa.Majani ya muhogo pia huliwa kama mboga za kijani zinazotoa vitamini A na B.

 

0
No votes yet
Your rating: None