Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Wadudu na magonjwa ya Mihogo

Wadudu waharibifu wanaoathiri muhogo pakubwa barani Afrika ni nyenyere wa kijani wa muhogo,cassava mealybug na panzi aliyechujika.Magonjwa makuu yanayoathiri muhogo ni ugonjwa wa cassava mosaic,cassava bacterial blight,ugonjwa wa casava anthracnose na kuoza kwa mzizi.Wadudu waharibifu na magonjwa,pamoja na mbinu mbaya za ukulima huungana kusababisha kupotea kwa mazao.

Uzalishaji wa muhogo hutegemea usambazaji wa vipande vya mashina vyenye ubora wa juu.Matatizo ya vipande vya mashina ya muhogo ni ya kwamba vipande hivi ni vizito na huharibika haraka kwani hukauka katika mda wa siku chache.

Kama zao la mzizi,muhogo huhitaji kiasi kikubwa cha kazi ili kuvuna.Kwani huharibika kwa urahisi,mizizi inafaa kutengenezwa kwa njia inayoiwezesha kuhifadhiwa pindi tu inapovunwa.

Aina nyingi za muhogo huwa na kemikali kiasi.Kemikali hizi zinaweza kutolewa kwa kutumia ,mbinu tofauti za utengenezaji kama kukwaruza,kukaushwa juani na kuchachusha.

2
Average: 2 (1 vote)
Your rating: None