Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kulipa Ushuru Wako

Kama unaishi, kufanya kazi na kununua vitu nchini Kenya unalipa ushuru.

Kulingana na kiasi cha pesa unazopokea, unalipa ushuru wa mapato (PAYE) inayokatwa kwenye mshahara. Unapofanya ununuzi, unalipa ushuru wa thamani ya bidhaa (VAT) kwenye baadhi ya bidhaa. Pia unalipa ushuru huu kwa huduma ikiwemo simu yako, umeme, na maji. Kama wewe ni mlipa ushuru, msajiliwa, lazima urudishe ripoti za ushuru kwa Halmashauri ya Ushuru nchini (KRA) kila mwaka.

Kama unapokea mshahara zaidi ya shilingi 10,100 kila mwezi, lazima ulipe ushuru wa mapato. Mwajiri wako hukata ushuru na baadaye kuilipa kwa Halmashauri ya Utozaji Ushuru Nchini (KRA) kila mwezi. Kila mwisho wa mwaka wa ulipaji ushuru Halmashauri ya Utozaji Ushuru Nchini, itakutumia fomu la ripoti ya ushuru wa mapato - I.T.1. Utaijaza fomu hiyo na kuirudisha katika Halmashauri ya Utozaji Ushuru Nchini kabla ya makataha (siku ya mwisho).

Halmashauri hiyo pia itataini kama pesa unazolipa kila mwezi zinamaliza deni lao la ushuru. Na kama umelipa pesa kidogo, watakutumia bili ya pesa zilizosalia. Kama umelipa nyingi, watakurudishia pesa. Huenda umelipa kidogo kama una mapato mengi kuliko kutoka kwa ajira yako ambayo ni lazima kuilipia ushuru.

Lazima ulipe kiasi fulani cha fedha kwa mapato ya kuwekeza, ya rasilimali (Kama vile kodi au faida kuu) na katika hali yoyote ya mapato unayoweza kuwa nayo. Unalipwa kwa vitu kama gharama ya matibabu, au gharama ya kuendesha biashara ukiwa nyumbani kwako. Unaweza kubahatika na upate kwamba baada ya kutekeleza hayo, Halmashauri ya Utozaji Ushuru Nchini (KRA) hukupa pesa badala ya kutumi njia nyingine.

0
No votes yet
Your rating: None