Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Ukuzaji Wa Ndizi Za 'Tissue Culture' Meru

tissue culture banana

Ndizi zinazopandwa kwa kutumiwa mbinu ya Tissue Culture  sasa zimeanza kupandwa katika sehemu za mashambani katika wilaya ya Meru kwa minajili ya kupanua ukuzaji wa ndizi zenye mazao mengi katika mkoa wa Mashariki.

Ukiongozwa na wizara ya kilimo kupitia kwa mpango wa National Agriculture and Livestock Extension Programme(Nalep) ,mafanaikio yake wachanganuzi wanasema yataleta kiwanda cha biashara na kugeuza sehemu hiyo kutoka kwa uzalishaji wa kiwango kidogo wa ndizi za kupika na kuwa kiwanda chenye manufaa makubwa.

Ndizi zinazozalishwa kwa kutumia tissue culture ya mmea zinakuwa kwa haraka na zina ‘‘furaha kuliko ndizi zingine’,anasema bwana Francis Munyua ambaye ni mkulima mwenye umri wa miaka 43 na hutumia TC katika divisheni ya Abothuguchi.

Maafisa wa Nalep wanasema ‘lengo la mradi huu unaothaminiwa na SIDA ni kuwahamasisha wakulima wadogo wadogo kutumia nyenzo za kupanda ambazo ni safi na hazina magonjwa ama wadudu na zinazopatikana kwa kutumia mbinu za uzalishaji"

Kama ilivyo katika sehemu zingine nchini Kenya zinazopanda ndizi, jitihada za wakulima kuongeza uzalishaji huko Meru zimepata pingamizi la ongezeko la wadudu waharibifu na magonjwa katika mazao,ukijumuisha wadudu aina ya weevil, minyoo na ugonjwa wa Panama na Sigatoka nyeusi.

 ‘‘Hii hufanya ndizi kuwa ghali kwa mnunuzi’’, anasema Charles Kiarie mfannya biashara wa siku nyingi wa ndizi jijini Nairobi.
Charity Mariene, ambaye ni afisa wa Nalep katika wilaya ya Meru anasema:‘‘kutokana na ndizi za  tissue culture tuna nafasi ya kutengeneza kiwanda cha ndizi chenye faida kutoka hapa.Tunawahimiza wakulima kuchukua hatamu ya maendeleo haya’’. 
 
Wakulima katika sehemu iliyo muhimu ya Kiria, takriban kilometa 15 kutoka mji wa Meru wametengeneza kikundi katika kijiji kuendeleza tamaduni hii kupitia ziara ya mkulima hadi kwa mkulima ili kubadilishana mawazo zoezi ambalo linategemea mahitaji.
 
 ‘‘Soko ni nzuri kwa ndizi hizi na huchukua tu sehemu ndogo ya shamba,’’ anasema Munyua  ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kiria. Munyua amepanda mashina yake ya ndizi katika ploti inayotazama barabara.``Nilifanya hivi kimakusudi’’, anasema. ‘‘Kama mwenyekiti wa kikundi cha watu waliovutiwa na kilimo cha ndizi,mafanikio yangu yatawafanya wakulima wengine kuiga kile ninachokifanya’’. Ilhali ndizi za kienyeji huchukua hadi miaka mitatu kukomaa, Munyua ana furaha ya kwamba ndizi za tissue culture huchukua miaka miwili. ‘‘Ustawi wa ndizi ni wa juu sana na pembejeo zake ni chache,‘‘anasema Charity Kiritu,mratibu wa nje wa Nalep katika kijiji cha Kiria.

Mradi wa Nalep huko Meku unapata mafunzo yake kutoka kwa miradi ya majaribio katika mkoa wa Kati  kupitia kwa mwanasayansi wa humu nchini Dkt Florence Wambugu,ambaye amepsdhihirisha ya kwamba teknolojia ya  tissue culture ni ya kufaa ya inaweza kusimamiwa vizuri na wakulima wadogo wadogo.
 
 ‘‘Ndizi hizi zinahitajiika kwa wingi kwa sababu zinatumika katika mahoteli kwa kutengeneza kitindamlo,’’anasema Charity Kiritu mratibu wa nje katika divisheni ya Abothuguci. ‘‘Kwa kuleta teknolojia hii kwa wakulima na kisha kwa wafanya biashara tunalenga kuboresha upatikanaji wa chakula na mapato.’'
  
Wafanya biashara washaonyesha ari ya kununua ndizi zenye ubora wa hali juu.Kando na ndizi za kienyeji za kupika ambazo kwa  kawaida hupandwa Meru.‘‘Ndizi za tissue culture zinahitajika sana na sisi hulipa shilingi 240 kwa  kila mkungu,’’ anasema Kiarie.

Wanasayansi wanasema kuingizwa kwa teknolojia katika sekta ya kitaifa ya ndizi itawawezesha wakulima wadogo wadogo kupata faida kutoka kwa teknolojia iliyokuwa nje ya uwezo wao miaka michache iliyopita.

Wakulima wa Meru tayari wameanza kupata mapato kwa kuuza aina ya Grandnian iliyotengenezwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo nchini Kenya (KARI).

Ingawaje Ndizi ni moja ya vyakula vinavyojulikana sana na kuliwa na watu wengi barani Afrika na hutoa mapato ya nyumbani yanayohitajika sana kwa  familia zinazofanya ukulima mdogo, uwezekano wake kuwa haujatumiwa hadi kufikia upeo wake.Nchini Kenya ndizi ni aslimia 1.7 ya jumla ya ardhi yote ya kilimo na mazao yake ya wastani ni tani 14 kwa kila hekta.

0
No votes yet
Your rating: None