Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Mahitaji ya kukuza ndizi

Ndizi humea katika michanga tofauti tofauti,lakini kwa kawaida huhtaji udongo tifutifu wenye rutuba ambao una kina kirefu,unapotisha maji vizuri na una kiwango cha juu cha mboji ambao unaruhusu ukuaji wa mzizi.Ndizi huhitaji angalau kiwango cha juu cha virutubishi,haswa madini ya potashiamu ambayo hutolewa ardhini kila matuunda yanapovunwa na yanafaa kurudishwa udongoni ikiwa uzalishaji unapaswa kuendelewa.

Ndizi hupandwa kwa kawaida katika mashamba madogo katika boma.Upaliliaji ni kupitia uzalishaji usiohitaji kujamiana,kwa kutumia chipukizi wenye afya wa kimo cha kama mita 1.5 kwenda juu na kama centimeta 45 duara na kuachia nafasi ya mita 3 kwa 3.Inapopandwa,mazao kama maharagwe,mahindi na viazi vitamu vinaweza kupandwa kwa pamoja na mimea michanga ya ndizi na baadaye hutolewa katika kifungio cha kanopi. Miti mingine ya matunda kama jack fruit na paipai inaweza kupandwa pamoja na ndizi kama chanzo cha matunda na pia huzuia upepo.

Mtandazo wa majani katika shamba la ndizi ni utendaji wa sayansi ya uchumi wa kilimo unaopendelewa kwa sababu ya ukandamizaji wa magugu,uhifadhi wa unjyevu na uthibiti wa rutuba katika udongo.Majani ya ndizi yaliyokatwa na sehemu za mmea zilizobakia hutandazwa juu ya ardhi baada ya mavuno na kuongezea nyenzo kutoka mazao ya shambani,shamba lililoachwa bila ya kulimwa,kinamasi na samadi kutoka kwa mifugo.Kwa kawaida masalio nyumbani husambazwa karibu na boma na husababisha mwinamo wa rutuba ya udonjgo na husababisha mazao ya juu karibu na boma na mazao ya chini ubmali unapozidi kuongezeka kutoka kwa boma.

Rutuba ya udongo hujumuisha sura ya nje, asili ya kemikali na ya kibayolojia ya mchanga na huhusishwa na mbinu za usimamizi na mfumo wa upandaji wa mimea.Kiwango cha virutubishi katika shamba la ndizi huwa vya juu kuliko katika sehemu zingine za shamba,labda kwa sababu ya maswala kadhaa:mashamba yenye rutuba ya juu huchaguliwa kwa uzalishaji wa ndizi hapo awali,viwango vya kupotea kwa virutubishi kutoka katika shamba la ndizi unaweza kuwa wa chini na virutubishi huhamishwa kutoka katika sehemu zingine za shamba hadi katika shamba la ndizi sana sana kwa njia ya utandazaji wa majani.

Hata hivyo kurudisha mabaki pekee yake hautatoa majani ya kutosha kwa ajili ya utandazaji wa kuhifadhi unyevu na kujazwa tena kwa virutubishi.Kiwango cha virutubishi vilivyotolewa katika tunda ni zaidi ya vile vimezuia kusonga katika sehemu zingine juu ya udongo.Kwa hivyo asilimia kama 86 ya wakulima wa ndizi katika eneo linalozunguka ziwa Victoria huongeza mabaki ya ndizi na nyongeza ya pembejeo.Inaweza kuonekana ya kwamba wakulima wanaoongeza masalio ya mazao ya shambani na samadi ya ng’ombe hupata mazao zaidi na yanawakilisha nyongeza ya asilimia 55 kwa masalio ya ndizi pekee yake.

Kupanda ndizi na mazao mengine ni jaribio la kawaida la kuboresha rutuba katika shamba,na ikifanyika huwa ni manufaa ya upili kwa lengo la msingi la utendaji huu. Mimea inayodumu kwa miaka mingi inaweza kupandwa kwa pamoja na ndizi kwa kujirudia kwa virutubishi kutoka kwa unyevu kwa sababu ya mfumo wa mizizi kupitia kwa kuanguka kwa matawi na mashina. Maharagwe ni zao la kila mwaka ambalo huhusishwa na ndizi. Mazao haya mawili yanawiiana kwa sababu maharagwe hayang’ang’anii virutubishi na ndizi iliyoko juu ya odongo na pia huhimili kivuli kuliko mazao mengine.

0
No votes yet
Your rating: None