Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Magonjwa na wadudu waharibifu wa ndizi

Mazao ya ndizi yanaweza kupunguzwa kwa hadi asilimia 100 kwa sababu ya wadudu waharibifu na uvamizi wa magonjwa na maambukizi.Wadudu waharibifu na magonjwa yanaweza kuzingatiwa kuwa kiamuzi kikuu cha tatu kwa zao la ndizi baada ya tabia ya sayansi ya uchumi wa kilimo ya cultivars na rutuba ya udongo.Mdudu anayejulikana kama Weevil ya ndizi (Cosmopolites sordidus) na minyoo wadogo ambao hawawezi kuonekana kwa macho makavu(radopholus similes) kuoza kwa mzizi hutokea kuwa wadudu waharibifu muhimu katika mchanga na pia magonjwa katika ndizi zilizoko katika eneo la ziwa Victoria.

Uvamizi wa wadudu umetajwa kuwa moja ya vipengele vinavyosababisha kupungua kwa mazao ya ndizi za kupikwa kupitia kuzuia kuimarika kwa mmea na hufupisha maisha ya ndizi.Uharibifu wa mmea hufanyika na kiluwiluwi kinachojenga mtaro ndani ya shina ukoka na kupunguka kwa zao huongezeka zao linapozidi kukua.Athari ya uharibifu wa mdudu huyu hufanyika kwa wakati mmoja na kupotea kwa rutuba katika udongo.Utendaji wa kawaida wa kuthibiti wadudu hawa aina ya weevil ni kung’oa shina liloko ndani ya mchanga la ndizi iliyokwisha vunwa na mashina bandia kama njia ya kuwanyima mahali pa kuzalisha.

Kuoza kwa mzizi kunakosababishwa na minyoo husababisha kung’ooka na hupunguza uzani wa mkungu wa ndizi.Utafiti umeonyesha ya kwamba uharibifu husababishwa haswa na kung’ooka ni zaidi kuliko kupunguka kwa uzani wa mkunga.Ni utendaji wa kawaida ya kwamba usimamizi wa rutuba katika udongo wa kutandaza ili kupunguza kupotea kwa unyevu kutoka ardhini kwa kutumia masalio ya viumbe hai unaweza kufidia kwa uharibifu unaoletwa na ukandamizaji wa minyoo kwa kuchachawisha na kuboresha ukuuaji wa mzizi,kuongeza idadi utendaji unaosaidia viumbe vya mchanga vinavyopambana na minnyoo hawa ama vinavyotoa mchanganyiko unaoua minyoo.Badala yake kabla ya kupandwa, chipukizi za ndizi zinafaa kuchemshwa ndani ya maji yenye chumvi.Hii ni mbinu ambayo ni ya kawaida katika Nyanza ya Kusini,ambapo maji moto ya chumvi hutumiwa na chipukizi huzamishwa ndani yake kwa dakika 5 hadi 10 na kuua viumbe hai vilivyo na manufaa na vile viharibifu vilivyoko kwenye mizizi ya chipiukizi ya ndizi.

Usimamizi mzuri wa shamba la ndizi ni mojawepo ya njia za uhakika za kuhakikisha una chakula cha kutosha na mapato zaidi kwa mwaka mzima.

0
No votes yet
Your rating: None