Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Kutunza Bajeti Yako

Kipengee cha bajeti nzuri ni iwe rahisi na kuweka rekodi nzuri. Kama jinsi ulivyo fanya ulipoanza kutengeneza bajeti itakubidi ufuatilie vile pesa zako mahali unapopata na pale zinapokwenda. Tumia njia ambayo inakufaa kwa kuandika kwa kitabu jinsi unavyotumia pesa zako au uweke risiti ya vitu unavyonunua.

Ripoti ya benki
Kama uko na akaunti ya hundi au akaunti ilioko, benki yako itakutumia ripoti yako ya matumizi kwa njia ya posta kila mwezi. Chunguza ripoti yako kwa njia ya makini na uangalie jinsi ulivyotumia pesa zako. Ukiona kuna jambo hufahamu, pigia benki yako simu uulize. Ikiwa unatumia hundi kulipa bili zako, weka rekodi ya kitabu cha hundi ili ufuatilie pesa ulizolipa na uliyemlipa, kisha ulinganishe na ripoti ya benki.

Ikiwa una akaunti tofauti, unaweza agiza kutoka kwa mtambo wa ATM, taarifa fupi ya matumizi yako ijulikanao mini-statement.

Kulipa ukitumia kadi
Ikiwa unatumia kadi ya ATM au kadi ya mkopo kununua bidhaa, hakikisha umeweka risiti ili uhesabu pesa unazotumia. Unapaswa kuweka risiti za kadi ya ATM ili uwe unafahamu kila wakati akauti yako ina pesa ngapi.

Linganisha matumizi yako ya kila mwezi
Kila mwisho wa mwezi, jaribu kulinganisha matumizi yako kwa bajeti yako. Weka matumizi yako katika mpangilio na utafute njia za kupunguza matumizi yako.

Jipe moyo kama unashindwa kufuata bajeti yako katika miezi ya kwanza. Utachukua muda kuwa na mpangilio unaofaa. Ikiwa unapenda kununua vitu kiholela, tafuta usaidizi wa kutii bajeti kutoka kwa marafiki na familia.

1
Average: 1 (2 votes)
Your rating: None