Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Maelezo

apple mango

Mwembe ni mti wenye ukubwa wa wastani hadi mkubwa na una rangi ya kijani kibichi kila wakati.Mti huu huwa na maua ya rangi ya waridi hadi nyeupe yaliyozaliwa katika vishada vya maua sana sana kutoka Disemba hadi Aprili. Ingawaje umbo na ukubwa wa tunda hutofautiana,mengi yao huwa aidha na rangi ya kijani, manjano ama nyekundu.Matunda yanaweza kuiva yakiwa mtini lakini ili kuzuia uharibifu kutoka kwa ndege na popo ama kuanguka ardhini,yanafaa kuvunwa pindi tu yanapokomaa. Hili huonekana kwa tunda kubadilika rangi kutoka rangi ya kijani hadi ya manjano.

Kuna aina nyingi,lakini zile maarufu za kienyeji ni Kidney,Julie Manzano na baadhi ya aina za Florida. Tunda la embe hutumiwa katika njia nyingi,lakini ulaji wake likiwa bado bichi ndilo jambo muhimu.Nyama ya tunda ni tamu na pia ina virutubishi. Ni chanzo cha vitamini A na C,na pia lina kiasi cha wastani cha thiamin na niacin na asilimia 10 hadi 20 ya sukari.Maembe pia yanaweza kugandishwa, kukaushwa, kuwekwa kwenye mikopo ama kupikwa katika jemu, jeli, vihifadhi, pai, achari na aiskrimu.

0
No votes yet
Your rating: None