Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Udongo Na Tabia Ya Nchi

Maembe humea na kutunda vizuri katika udongo wenye kina kirefu,unaopitisha maji vizuri na una rutuba lakini utamea na kuzalisha katika aina tofauti za udongo. Mmea huu una mfumo wa mizizi wenye nguvu ambao unaweza kupenya katika eneona kuchukua virutubishi. 

Kuna uwezekano wa kutokea tatizo katika udongo ulio na Caliche ama chokaa na hutokea katika visiwa vya Virgin lakini matatizo haya yanaweza kumalizwa kwa kuutibu mchanga na madini kama chuma,zinki,manganisi(angalia uwekaji mbolea). Mmea huu utamea vizuri katika mvua ya baina inchi 30 hadi 100 kwa mwaka,lakini kwa uzalishaji kamilifu wa wa matunda kipindi kirefu cha ukame mkali kinahitajika.

Maembe huathirika kwa urahisi na uzalishaji usio wa kawaida na unaofanyika baada ya miaka miwili na tabia hii hutofautiana kulingana na aina. Ingawaje chanzo na utatuzi haujapatikana kwa hii hali ya tabia ya nchi lakini linaonekana kuwa na athari kwa sifa bainifu ya embe. Ikiwa msimu wa kiangazi utakuwa mkali na mrefu zaidi tabia ya mmea kuzalisha itakuwa ya kawaida. Unyunyizaji na Potassium nitrate (angalia uwekaji wa mbolea) unaweza kutumika kulikabili tatizo hili la kuzalisha baada ya kila miaka miwili katika mimea inayoweza kudhurika kwa urahisi (kwa mfano Haden).

0
No votes yet
Your rating: None