Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Wadudu Waharibifu

Maembe kwa kawaida huwa hayaathiriki na wadudu waharibifu.Mara chache kunaweza kutokea vamizi la wadudu kama magamba,nyenyere,aphid ama thrips.Kwa miti michanga uoshaji ulio kamilifu na sabuni isiyo kali ama kutia Malathion ama ugiligili nwa mafuta ya Diazinon plus(Mafuta ya Volck) kwa kawaida hutosha.Wakati athari kubwa inapotokea unaweza kung’amua ugonjwa wa kuvu ya Anthracrose ambao unaweza kuwa tatizo kubwa kwa mwembe.Kuvu hii husabisha madoa meusi kwenye.majani,maua na matunda.Maua na matunda madogo kuliko ilivyo kawaida yaliyoathirika hupukuswa na zao.lote linaweza kupotea.

Tunda lililokomaa linaweza kuwa na madoa ya kubambuka na hata matunda yanayonekana kuwa safi yatakuwa na madoa ya anthracnose yatakopoiva. Anthracnose inaweza kuepukika kwa kupanda miti katika sehemu zilizo wazi na zinapitisha maji kwa uzuri na zina mzunguka huru mzuri wa hewa na unyevunyevu kwenye hewa amabao ni wa kudumu katika msimu wa kutunda.

Maeneo yenye msimu mrefu,wa kiangazi zinafaa wakati wa kutunda na vile vile kuthibiti anthracnose.
Uwekaji wa nafasi ya kutosha ili kuzuia msongomano wa miti pia husaidia katika uthibiti.Uthibiti wenye mafanikio wa ugonjwa huu unaweza kupatikana kupitia viua wadudu vyenye Zineb,Maneb na
Shaba.

Vipele vya maembe pia husababishwa.na kuvu.Madoa yanayosababishwa na kuathirika kwa majani ni madogo,membamba na huwa na rangi ya hudhurungi nzito hadi nyueusi.Kwenye matunda,madoa ya hudhurungi yasiyo ya kawaida hutokea na huwa kama koki na hupasuka.Vipele havina ukali na sio vya kawaida katika maembe kama ilivyo anthracnose.Vioevu vya shaba vinashauriwa katika kuthibiti vipele.

3
Average: 3 (1 vote)
Your rating: None