Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Uvunaji / Uhifadhi

Aina nyingi zinaweza kuchunwa siku kadhaa kabla ya kuiva na ziwe na ubora wa hali ya juu.Embe la Julie ni lazima lichunwe linapokaribia kuiva ili,kupata ubora wa juu ili mti mahsusi uweze kuvunwa kwa kipindi cha siku 2 hadi 3.

Matunda yanafaa kuchunwa na mkono na kushikwa kwa upole wakati wote ili kuzuia kuvilia.Mifuko yenye vipini virefu inaweza kutumiwa kuchuna matunda kutoka juu ya miti.Baada ya kuchuna,matunda yanafaa kupakiwa katika mitungi (ya plastiki ama mbao)ambayo haiwezi kukunjika ya Ib 30 amabayo imelainishwa na nyenzo kama majani makavu ama polyfoam.Madoa ya anthracnose kwenye matunda yaliyoiva yanaweza kutokea na hili huharibu sura ya matunda na kuyafanya kutoweza kuuzika.Tatizo hili linaweza kupunguzwa ama kumalizwa kwa kutibu matunda na maji moto baada ya kuyavuna katika hali joto ya farenihaiti124 hadi 125(centigredi 51 hadi 51.5) .kwa dakika 15.Hali joto na mpangilio kwa mda katika matibabu haya ni muhimu sana.

Ukipitishwa jeraha kwa tunda litatokea na pia matibabu haya hayana matokeo mazuri ikiwa hali joto na mda unaofaa hauja wekwa maanani.Utafiti wa hivi karibuni katika kituo cha majaribio ya kilimo UVI(AES)

Unaonyesha ya kwamba unyunyizaji wa majani na asilimia 4 hadi 6 ya KNO3 ukifanyika kuanzia miezi ya Septemba hadi Novemba kabla mti haujatoa maua huzalisha maua na matunda yaliyolingana.

Maembe yanaweza kuhifadhiwa katika jokofu kabla hayajiava katika hali joto ya farenihaiti 50 (centigredi 10) na baada ya kuiva baina ya farenihaiti 45 hadi 50 (centigredi 7.2 hadi 10).  Hali joto zilizo chini kupita hizi husababisha mzizimio ambayo hufanya matunda kutoiva vizuri,madoa ya anthracnose na dosari zingine za ngozi.

0
No votes yet
Your rating: None