Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Ng'ombe Wa Airshire

Airshire

Ng’ombe wa Airshire wana rangi ya hudhurungi na madoa yanayofanana na viraka meupe. Huwa wakubwa kwa umbo na wana uzani wa kama kilo 450.

Huzalisha maziwa kwa wingi, kama lita 30 kila siku. Maziwa ya ng’ombe wa Airshire yana kiwango cha mafuta ya siagi cha 4.0%.
 
Ng’ombe wa Airshire ni wenye nguvu na wanaweza kustahimili katika mazingira yanayotofautiana. Hata hivyo, wanahitaji chakula kingi cha kama kilo 90-110 cha chakula kibichi na lita 60 za maji safi kila siku. Kwa hivyo, wanaweza tu kufugwa katika sehemu zenye maji na lishe ya kutosha.

Tofauti na ng’ombe wa Fresian, Airshire wanaweza kuachiliwa huru katika malishoni.

 

0
No votes yet
Your rating: None