Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Ng'ombe Wa Borana

Boran

Ng’ombe wa Borana huwa wa rangi ya hudhurungi hadi kijivu kwa umbali au huwa na madoadoa.Wana mwili wa wastani hadi mdogo na kwa kawaida huwa na uzani wa kilo 350-400. Ndume huwa wakubwa kuliko jike. Kwa tabia ni wapole na hukaa katika kundi hali ambayo huongeza usalama wao katika mbuga za Afrika ambako wafugaji wa kuhama hama hutembeatembea.

Hufugwa kwa ajili ya nyama na maziwa. Utoaji wao wa maziwa ni wa chini na hauna uwezekano wa kibiashara. Hata hivyo maziwa yake yana kiwango cha juu cha mafuta ya siagi cha 4.8%

Ng’ombe wa Borana ni wa asili ya Ethiopia na walifugwa na jamiii zinazoishi mpakani mwa Kenya, Ethiopia na Somalia. Hata leo, ndio aina ya ng’ombe wanaofugwa sana katika eneo hili kame. Wafugaji wa kuhamahama hupendelea Boraan kwa sababu wana miguu yenye nguvu na wanaweza kutembea umbali mrefu.

Huhimili ukame. Hii inamaanisha wanaweza kuishi kwa lishe kidogo na hupata nafuu kwa haraka baada ya ukame. Huhimili magonjwa kwa sababu ngozi zao ni nyororo kwa hivyo kupe hupata ugumu wa kushikilia. Borana wanaweza kuhimili joto na kuishi vizuri katika sehemu kame.

Ng’ombe wa Borana wana wepesi wa kubadilika kulingana na mazingira wa hali ya juu na wameweza kustahimili hali za nchi tofauti na zile za sehemu kame zilizoko kaskazini mwa Kenya na Ethiopia.

Nchi ya Kenya ilizalisha ng’ombe wa Borana aliye bora kijenetiki na ni yule ambaye ameuzwa kwa nchi kama Afrika Kusini, Zambia,Tanzania, Uganda, Marekani na Australia.

0
No votes yet
Your rating: None