Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Ng’ombe wa Jersey

Jersey

Ng’ombe wa Jersey wana rangi ya hudhurungi-kijivu na huwa na doa la kijivu haswa kwenye shingo na kichwa.Macho yao huwa ni kama yanatoka nje.Huwa ni wadogo-wana ukubwa wa wastani na uzani wao huwa ni kilogramu 350.

Hufugwa kwa ajili ya maziwa.Uzalishaji wao wa maziwa ni wa wastani na hutoa lita 20 kila siku.Maziwa yao yana kiwango cha juu cha siagi cha kama 5.2%.

Hawahitaji chakula kingi sana na mahitaji yao ya kila siku ni kama kilogramu 65-85 za chakula kibichi.Ng’ombe wa Jersey huwa sugu na wanaweza kuishi katika hali za nchi tofauti.Hata hivyo huathirika kwa urahisi na homa ya maziwa na magonjwa yanayosababishwa na kupe.

Wanapendekezwa kwa uzalishaji mtambuka ili kuboresha vizazi vya hapa nyumbani kama Zebu na Boran.

 

0
No votes yet
Your rating: None