Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Ng'ombe wa Sahiwal

Sawihal

Sahiwal ni ng’ombe wenye nundu na waliletwa Afrika kutoka India na Pakistan.Wanatofautiana kwa rangi kutoka nyekundu-hudhurungi hadi nyekundu yenye rangi nyeupe kidogo katika shingo na sehemu ya chini.

Sahiwal huwa wakubwa na huwa na uzito wa kama kilogramu 350-400.Hufugwa kwa ajili ya nyama na maziwa.Ndio wanaotoa maziwa mengi katika wale ng’ombe wenye nundu lakini uzalishaji wao wa maziwa ni wa chini kwa ajili ya kibiashara.Hata hivyo,wana kiwango cha juu cha mafuta ya siagi cha 4.8 %.

 Ng’ombe wa Sahiwal hupendwa kwa sababu wanaweza kuishi kwa urahisi katika sehemu sizizo na rutuba kama maeneo kame.Huweza kuhimili wadudu kama kupe na pia joto jingi.Katika Afrika ya Mashariki ng’ombe hawa hufugwa katika shamba la mifugo katika sehemu zilizo kauka na pia hufugwa na jamiii za kuhama hama.Ni ngumu  kuwazalisha kwa sababu hupendelea kujamiana usiku.

 

0
No votes yet
Your rating: None