Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

  • Kuvuna maji kwa kutumia kinga za udongo

Kuvuna maji kwa kutumia kinga za udongo

Kuna njia nyingi tofauti za kuteka maji ya mvua.Watu wengine huteka maji ya mvua kutoka kwa paa na kuyaweka katika matangi ya maji.Watu wengine hujenga mabwawa,ama huteka maji katika mashimo yasiyo na kina kirefu,matuta ya mkingamano na majenngo mengine madogo.Maji hupatikana kwa urahisi kwa matumizi wakati wa msimu wa ukame.Maji yaliyotekwa katika msimu wa mvua yanaweza kuhifadhiwa juu ya ardhi-matangi,mabwawa na makontena.Ama yanaweza kuhifadhiwa chini ya ardhi.Ujenzi wa kinga za udongo ni mojawapo wa njia za kuhifadhi maji chini ya ardhi. 

Makala haya yanaeleza jinsi ya kujenga mfululizo safu wa kinga za udongo katika shamba ili kuvuna maji ya mvua ambayo yanaweza kutumiwa mwaka mzima kupanda mimea na katika matumizi ya nyumbani.Mashimo katika udongo ni muhimu kwa sababu humsaidia mkulima kupanda mimea kote katika msimu wa kiangazi,wakati maji ni machache.hufanya kazi kwani huteka maji ya mvua na kuyahifadhi ndani ya udongo.

Lakini ni njia gani mashimo katika udongo huhifadhi maji katika mchanga?Kinga za udongo zinaweza kufanya hili kwa ajili ya njia zilizojengwa.Yanafaa kujengwa katika sehemu ya chini ya mteremko usio mkali.Wakati maji ya mvua yanateremka chini ya mteremko,mashimo katika udongo hupunguza kasi ya maji ili yavuje ndani ya udongo badala ya kupita juu yake na kwa njia hii mimea hupata maji zaidi.

Jinsi ya kujenga kinga za udongo

Kinga za udongo kwa ufupi ni vilima vya udongo.

  1. Chimba mtaro wenye kina kifupi,kisha jaza udongo uliotoka kwenye mtaro kujenga kilima cha mviringo ambacho ni laini.Kilima hiki kinafaa kuwa na kimo cha kama centimeta 15 hadi 30 kuenda juu.Mtaro na shimo katika udongo linaweza kuwa na upana wa mita kadhaa. 
  2. Maji yanapokimbia chini ya mlima wakati  wa msimu wa mvua,huenda kwa kasi ya chini yanapofikia kinga za udongo na huvuja hadi ndani ya ardhi.Kwa hivyo udongo katika shamba huwa na unyevu na hili hufanya mimea kuwa na nguvu.
  3. Kiwango cha maji katika kisima huongezeka na pia kinakweza kutumiwa kusambaza maji ya kunywa na kunyunyizia katika mboga wakati wa msimu wa kiangazi.Kwa njia hii shamba huwa la kijani kibichi kwa mwaka mzima.

Ni muhimu kufahamu ya kwamba mteremko unafaa kuweko ili maji yakimbie chini ya kilima.Lakini mteremko huu haufai kuwa mkali ama maji ya mafuriko yataosha kinga ya udongo.Mteremko usio mkali hufaa.Hata hivyo kukiwa kuna kijito kwenye ardhi,maji mengi zaidi yanaweza kutekwa katika ardhi viile vile.Kinga za udongo zinaweza kumomonyoka kupitia maji ya mvua na maji yanayopita juu ya ardhi,kwa hivyo urekebishaji unahitajika kuweka mchanga mahali pake.

Kabla ya kujaribu kutengeneza bwawa la udongo,kwa kawaida ni jambo la busara kuangalia na ujaribu kumpata mtu ambaye ashajenga bwawa la udongo.Kwa kuwauliza wakulima wengine ikiwa wanajua watu waliojaribu huboresha mafanikio ya mradi kwa kiasi kikubwa.

 

1
Average: 1 (1 vote)
Your rating: None

Maji are available for use during the season and me.Maji yaliyotekwa in the rainy season can be stored on land-tanks, reservoirs and makontena.
From: Yeast Infection Review

»