Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Saratani ya Matiti

Wanawake walio hatarini kuupata ugonjwa huu ni:

 • Ajuza
 • Wenye asili ya kihindi au kizungu
 • Wanawake ambao washaugua saratani ya matiti mbeleni
 • Walio na jamaa wa karibu ( mama,dada,binti) ambao washawahi kuuguwa ugonjwa huu
 • Wanawake wenye hitilafu ya kinasaba kutoka kwa mzazi aliyeugua ugonjwa huu
 • Wanawake tasa au waliowapata watoto baada ya umri wa miaka 30.
 • Wanawake waliopata damu yao ya hedhi wakiwa na umri mdogo kabla miaka 12.
 • Wanawake waliokatika hedhi wakiwa wamechelewa baada ya miaka 50.
 • Wanawake wenye matiti makubwa(daktari anaweza kukuelezea baada ya uchunguzi wa mammogram)
 • Wanawake waliotumia tembe za uzazi,waliokosa kunyonyesha, wanaokunywa pombe kila siku,wanaonenepa sana baada ya kukatika hedhi,wanaomeza vidonge vya kubadilisha nasaba,na wale ambao hawakunyonyesha.

Dalili ya saratani ya Matiti:

 • Uvimbe kwenye matiti au kwapa
 • Mabadiliko katika umbo la matiti
 • Chuchu kutoa usaa ama titi kuwa nyororo
 • Chuchu kupotelea ndani ya matiti badala ya kujitokeza nje
 • Madutamaduta kwenye matiti kama yale ya maganda ya machungwa
 • Kubadilika kwa ngozi ya matiti na chuchu kuonekana zimefura

Ukiwa na mojawapo ya dalili hizi muone daktari,ni vyema kufanyiwa uchunguzi wa mammograms.

Fanyiwa uchunguzi wa matiti mapema ili kutambua saratani ya matiti mapema.Kujichunguza kila mwezi na kufanyiwa uchunguzi wa mammograms mara moja kwa mwaka hasa wanaozidi miaka 40 in bora.

2.916665
Average: 2.9 (12 votes)
Your rating: None

I think that thanks for the valuabe information and insights you have so provided here.
linkedin careers

»