Kuweka akiba ni njia bora ya kupangia kununua kitu. Ni njia pia ya kujiandaa japo ukapatwa na jambo la dharura au ungetaka kunua kitu ghali bila kukopa.
Kuweka Akiba
Huchukua muda mfupi: Unapoanzia kuweka akiba hadi utakapotumia inachukua kati ya miezi 6 hadi miaka miwili.
Inakuzuia kutumia pesa ovyo: Usifikiri ukiweka akiba hutawahi kutumia hiyo pesa. Kuweka akiba ni kuweka pesa kando SASA hivi ili uitumie BAADAYE.
Inakupa utulivu: Kuwa na Akaunti ya akiba ni salama kuliko kuweka pesa zako chini ya kitanda. Benki na SACCO zina bima ya kulinda pesa, hakikisho kwamba pesa zako ziko salama.
Je kwa nini kuweka akiba ni muhimu?
Kuweka akiba ni muhimu kwa sababu kuwa na pesa ya ziada hukupa utulivu na kukuwezesha kununua vitu bila kukopa.