Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Pesa za Kukopa

Haimaanishi “pesa za bure”; Mkopo ni pesa unayoomba na ni lazima urudishe! Wakati mtu anakupatia pesa utakayoirudisha na faida juu yake, amekupatia mkopo. Riba huwa ni gharama ya kuomba pesa – ni kiasi cha pesa zaidi unacholipa kwa sababu ya kuweka pesa za aliye kukopesha.

Ikiwa una akaunti ya benki au SACCO na una bajeti ambayo unafuatilia vizuri, basi uko tayari kuwa na kadi ya mkopo. Si vizuri kuchukua kadi ya mkopo au mkopo ikiwa huna bajeti unayofuatilia.

Malipo
Ukilipa wakati ufaao, inaonyesha kwa ripoti yako ya mkopo. Ukikosa kulipa, unatozwa ada ya kuchelewa na yote huanishwa kwa ripoti yako. Njia nzuri ya kukata matumizi ya kadi ya mkopo ni kutokuwa na kadi nyingi na usiwe unaibeba kila wakati. Beba kadi wakati unaenda kununua kitu fulani. Ukiweka kadi kwa mfuko kila wakati ndio utavutiwa kuitumia kununua kitu ambacho hukuhitaji.
 
 

 

3.333335
Average: 3.3 (3 votes)
Your rating: None