Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Ni Daktari Yupi Nahitaji?

Stethoscope

Kila mtu anahitaji daktari au muuguzi wa kumpa ushauri kuhusu afya yake kila mara. Shida: Mtaalamu unayemuhitaji kukukagua na kutibu ugonjwa ulionao yaweza kuwa shida kumpata ikiwa hufahamu magonjwa wanayoyatibu. Unapofahamu chanzo cha magonjwa, utaweza kupata afya bora unayohitaji.

Kwa hivyo hebu tuwagawanye Madaktari katika sehemu mbili: Wauguzi wa kimsingi na Wataalamu.

Madaktari wakuu.

Madaktari wengi hutoa huduma za kimsingi: Utawatembelea wauguzi hawa mara kwa mara:

Madaktari wa kijumla: Hawa ni madaktari wanaotoa huduma za afya kwa jamii nzima, au wanafahamu ni mtaalamu yupi anayeweza kutoa usaidizi unaohitaji.Wao hukuchunguza, hukupima, hutoa chanjo na kuzuia maambukizi, virusi na kadhalika.

Madaktari wa meno: Hawa ni madaktari waliona utaalamu wa afya ya kinywa chako na meno .Wanaweza kukutuma kwa wataalamu wengine wa magonjwa na matibabu ya kinywa na meno yako

Madaktari wakufunzi: Daktari mkufunzi ni daktari anayeshughulikia afya ya watu wazima pekee.

Madaktari Wakunga: Hawa ni wataalamu wa sehemu nyeti za kike na afya ya uzazi.Utamuona mkunga unapohitaji uchunguzi wa fupanyonga au ukiwa na matatizo sehemu za uke, au ukiwa mja mzito na unahitaji uchunguzi kabla na baada ya kujifungua.

Madaktari wa watoto: Madaktari hawa hushughulikia afya ya watoto wachanga na vijana.Huwapa watoto nguvu za mwili, chanjo na kuwapa ukaguzi wa kiafya.Wao pia huwaelekeza kwa wataalamu zaidi wa watoto.

Wataalamu wanapochukua jukumu.
Muuguzi wako yuwaweza kukuelekeza kwa mtaalamu, daktari aliye na tajiriba na mafunzo ya juu ya utaalamu Fulani.Kwa hivyo usiwe na shaka unapoambiwa ukamuone mtaalamu.Ni wajuzi wa sehemu tofauti za mwili wa binadamu kutoka kwa madaktari wa ngozi mpaka kwa madaktari wa moyo huhakikisha ikiwa mtaalamu wako ana cheti cha kuhudumu kutoka kwa halmashauri ya wauguzi.

Kumbuka, utakapohitaji mtaalamu, wataalamu wengi hawataweza kukukagua hadi atakapohakikisha kuwa umetumwa kwake na muuguzi wa afya za kimsingi. Kampuni nyingi za bima haziwalipi wataalamu iwapo hukuelekezwa na muuguzi wa afya za kimsingi.

Kwa hivyo ukielekezwa kwa wataalamu, tizama orodha hii ya wataalamu ujifahamishe zaidi kuhusu wanachotibu, na uwe umejitayarisha kwa miadi nao.

3
Average: 3 (1 vote)
Your rating: None