Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Meno ya watoto

Watoto wenye meno nzuri hukua kuwa watu wazima wenye meno nzuri. Ukiwafunza watoto wako jinsi ya kusugua meno na kutoa uchafu katikati ya meno kwa kutumia uzi spesheli, isitoshe pia kuwapeleka kwa daktari wa meno mara mbili kwa mwaka watakua na meno nzuri na yenye afya
Hata kama meno ya watoto wako itang’oka kisha mengine yamee ni muhimu sana kuyaweka yakiwa safi. Meno ya mtoto wako mchanga huwa katika sehemu muhimu ambazo meno mengine yatamea vizuri akiwa mtu mzima.
 
Watoto wadogo:
Watoto wako wanapaswa kujifunza kuhusu utunzi bora wa meno kutoka kwako kwa mfano mwema kwa kusugua meno, kuondoa mabaki ya vyakula kwenye meno kwa kutumia uzi spesheli. Wasaidie kusugua na kuondoa vyakula kwenye meno hadi wafikishe umri wa miaka 7 ama 8 ambapo wanaweza kutekeleza wenyewe. Hapa pana njia zitakazoweza kukusaidia.
 
  • Tumia mswaki ya mtoto iliyo laini na utie kiasi kidogo cha dawa ya meno iliyo na floraidi
  • Fuata maagizo jinsi ya kusugua meno ya mtoto wako lakini tekeleza haya kwa upole
  • Hakikisha kuwa umesugua meno ya mtoto wako kwa dakika mbili
  • Hakikisha kuwa mtoto wako amesuuzia mdomo wake na kutema dawa ya meno. Usiwache waimeze
  • Usisahau kuondoa vyakula katikati ya meno kwa kutumia uzi spesheli.
 
Hakikisha kuwa mtoto wako anatekeleza tabia hizi njema. Usiwaache wanywe vinyaji vingi baridi au vinyaji vya sukari. Hapa kwa wingi tunamaanisha zaidid ya moja kwa siku. Epukana na tabia ya kumpa mtoto wako vinyaji baridi na vyakula. Haya waweza kufanya mara moja tu. Unywaji wa vinyaji baridi ni mbaya kwa meno ya mtoto wako na ukuaji wake.
 

 

0
No votes yet
Your rating: None

It’s appropriate time to make some plans for the future and it is time to be happy. I have read this post and if I could I wish to suggest you few interesting things or advice. Perhaps you could write next articles referring to this article. I desire to read even more things about it!
scentsy light bulb

»