Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Masomo ya juu

Kupata shahada inamaanisha unaweza kupata kazi ya malipo mazuri, ikiwezekana kazi yenye dhamana nzuri na mapato mengi. Anza mipangilio ukijitayarisha kwenda chuo kikuu, vivyo basi uchukuwe masomo sahihi kwa ujuzi unaotaka kunyanya baadaye, na upange vile utaweka fedha za masomo yako. Pata maelezo hapa kuhusu taasisi tofauti za elimu ya juu katika nchi yako na vile utaanza mpango.


Chagua wapi pa kusomea
Tafuta vyuo vikuu gani, vyuo vya ufundi na vyuo vya mafunzo vilivyoko katika nchi yako.
Kulipia masomo ya juu
Masomo ya juu yako ghali kwa bahati nzuri, unaweza pata usaidizi kulipa baadhi ya karo au yote.

Kalenda ya mpangilio
Tumia kalenda yako kama mwongozo wa kupangia elimu yako ya juu.

Kufanya mtihani wa SAT ama ACT
Ikiwa ungetaka kusomea chuo kikuu au chuo cha mafunzo ya juu katika nchi ya kigeni, labda itakubidi ufanye mtihani wa SAT ama ACT. Pata maelezo kuhusu kujitayarisha kwa majaribio. Tafuta vile utakavyo jisajili na yanagharamia pesa ngapi.

Je unajua vyuo vikuu vingi wanakubalia wanafunzi waliopevuka (kupita umri wa miaka 23)? Unahitajika kuandika majaribio ya kiingilio kuona kama utaweza kuzoea na kazi.
Wasiliana na chuo kikuu utakachopendelea, kupata mengi zaidi.

Kuna hatua nyingi za kujitayarisha kwa masomo ya juu unaweza pata maelezo unayohitaji katika mzinga (Beehive) ama unaweza jifunza zaidi kuhusu shahada, diploma na chunguo mengineo ya elimu kwa mkufunzi wa kazi.