Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kilimo cha Mifugo

Ng’ombe, mbuzi na kuku ndio wanaofugwa sana na Wakenya. Mifugo mbadala kama sungura na batamzinga wameanza kuwa mashuhuri kwa vile wana nyama nyeupe ambayo ina afya kuu kwa binadamu. Watu ambao hapo mbeleni hawangepata samaki kwa sababu wanaishi mbali na mito na ziwa, siku hizi wanakula samaki waliofugwa kwa vidimbwi katika 'mashamba' ya samaki. 

Ikiwa unataka kupata faida kutoka kwa mifugo wako ni lazima uanze na uchaguzi wa mbegu nzuri ya wanyama, uwalishe vyema, uwakinge dhidi ya maradhi na uweke rekodi ya shughuli zote zinazohusiana na wanyama wako. Katika sehemu hii, utaelezwa yote yanayoambatana na ufugaji wa wanyama.